DKT. NCHIMBI KUUNGURUMA LINDI LEO
Na Mwandishi Wetu, Lindi
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi leo alasiri atazungumza na wananchi wa Mkoa wa Lindi kwenye mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika Uwanja wa Mpilipili mjini Lindi.
Dkt. Nchimbi na msafara wake wamepokelewa leo katika Ofisi za CCM za Mkoa, atafanya kikao na Kamati ya Siasa na mkutano wa ndani wa makundi mbalimbali.
Ziara hiyo ni maalum kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha katika Daftari la Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Novemba mwaka huu.
Kabla ya kuingia mkoani Lindi, Dkt.Nchimbi alimaliza ziara ya siku mbili mkoani Mtwara, ameongezana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndugu Issa Ussi Haji (Gavu) na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Rabia Abdallah Hamid.
No comments