Header Ads

ad

Breaking News

Bilioni 6.6 kutumika mradi wa ujenzi minara 45 ya mawasiliano Mkoa wa Kagera

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Moses Nnauye (Mb), alipowasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kuanza ziara ya kukagua ujenzi wa minara ya mawasiliano ya simu katika wilaya ya Muleba na Biharamulo mkoani humo Julai 16,2024

Na Mwandishi Wetu, WHMTH, Kagera

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote unatarajia kujenga minara 45 katika kata 44 yenye thamani ya sh. bilioni 6.6 za kitanzania katika Mkoa wa Kagera, kwa lengo la kuhakikisha mikoa iliyo pembeni inaungwanishwa na Tanzania ya Kidigitali,.

Hayo yamebainishwa Julai 16, 2024 na Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Bi. Justina Mashiba, wakati akitoa taarifa ya utendaji wa Mfuko katika Mkoa wa Kagera, mbele ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.) aliye katika siku ya pili ya ziara yake Mikoa ya Kanda ya Ziwa kukagua ujenzi wa Minara ya Mawasiliano ya simu.

Bi.Mashiba amesema minara hiyo 45 ya Kagera ni kati ya minara 758 inayofadhiliwa na Serikali kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka wa fedha 2023/2024 hadi 2024/2025 , ambapo kwa Mkoa wa Kagera ikitarajiwa kuwanufaisha Watanzania 801,961 itakapokamilika mwanzoni mwa mwaka 2025.

Amesema, Mkoa wa Kagera ni kati ya mikoa 26 Tanzania Bara, itakayonufaika na kwamba wilaya za mkoa huo inakojengwa minara 45 na idadi ya minara kuwa ni Biharamulo (13), Bukoba DC (1), Karagwe (14), Missenyi (3), Kyerwa (4), Muleba (8), na Ngara (2).

Amesema hadi kufikia mwishoni mwa Juni 2024, jumla ya minara kumi (10) imeshawashwa na Watoa Huduma za Mawasiliano.

Mtendaji Mkuu huyo wa UCSAF amesema, kupitia minara 10 iliyowashwa vijiji kadhaa vya wilaya hizo vimenufaika na mradi huo, katika kata 44 zikiwemo Kaniha, Nyakahura, Nyantakara, Nyarubungo, Igurwa, Kihanga, Kakunyu, Karambi na Ngenge.

Kwa ujumla tangu mwaka 2009 jumla ya minara 80 imejengwa katika wilaya saba (7) za Mkoa wa Kagera, kutokana na makubaliano kati ya Serikali, kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na watoa huduma za mawasiliano.

Bi.Mashiba amesema, minara hiyo iliyojengwa kwa teknolojia ya 2G, 3G na 4G, kwa ruzuku iliyotolewa na UCSAF, imegharimu jumla ya Shilingi Bilioni 10.89, na inawanufaisha Watanzania 1,248,911.

Ametaja wilaya 7 zinazofaidika na minara hiyo na idadi ya minara iliyojengwa, kwenye mabano, kuwa ni Biharamulo (15), Bukoba DC (5), Karagwe (22), Missenyi (14), Kyerwa (6), Muleba (4), na Ngara (14).

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Bi.Justina Mashiba akitoa wasilisho la hali ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa minara ya mawasiliano mkoani Kagera mbele ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Moses Nnauye, Kaimu Mkuu wa Mkoa Kagera, Mhe.Erasto Sima na viongozi mbalimbali wa mkoa huo, wakuuu wa taasisi na watoa huduma, Julai 16,2024 kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.

 
Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Wakili John Daffa akitoa wasilisho la hali ya huduma ya mawasiliano kwa Mkoa wa Kagera mbela ya 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Moses Nnauye (Mb) , Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Erasto Sima na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kagera, wakuu wa taasisi na watoa huduma chini ya ya Wizara Julai 16,2024 kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa

No comments