Header Ads

ad

Breaking News

BALOZI DKT.NCHIMBI ACHANGIA MILIONI 10 UJENZI OFISI YA CCM MTWARA VIJIJINI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, akizungumza na wananchi wa Kata ya Mpapura, Mtwara Vijijini.

Na Mwandishi Wetu, Mtwara

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiambatana na wajumbe wa sekretarieti ameendelea na Ziara yake mikoa miwili ya kusini ambayo ni Lindi na Mtwara Julai 29 Julai, 2024 amesalimia na kuzungumza na wananchi wa Jimbo la Mtwara Vijijini Kata ya Mpapura ambalo liko upinzani

Balozi Nchimbi alisema pamoja na kwamba, jimbo hilo liko upinzani lakini utekelezaji wa Ilani jimboni hapo ni wa kiwango cha juu kwani wameweka Kaimu Mbunge Mhe. Chikota anayefanya shughuli hapo, hakika kazi imefanyika nafikiri mmeona sasa kazi kwenu.

Alisema wakati ukifika ibidi mbadilike kwani mnapata maendeleo lakini hamna wa kumhoji pamoja na yote CCM inawafanyia mambo makubwa waliyoyasikia wenyewe, sasa wakati ukifika pigeni chini wasiobadilika kichagueni Chama Cha Mapinduzi.

Dkt.Nchimbi amewataka wananchi kuendelea kutunza na kulinda amani asitokee mtu akawadanganya kuhusu kuharibu amani iliyopo, ambapo alichangia shilingi milioni 10 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa ofisi ya Chama Wilaya Mtwara Vijijini.





No comments