Header Ads

ad

Breaking News

Watakiwa kufanyakazi kwa kujiamini, uadilifu na weledi

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya Kupiga Kura Jimbo la Kwahani Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar wametakiwa kufanya kazi kwa kujiamini, uadilifu na weledi wanapotekeleza majukumu yao ya uchaguzi kutokana na dhamana waliyopewa na Tume.

 Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt.Zakia Mohamed Abubakar wakati akifungua mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya vituo yanayofanyika kuanzia leo Juni 5 hadi 6, 2024 Skuli ya Sekondari ya Lumumba, Mjini Magharibi- Zanzibar.

 “Mnatakiwa kutambua kuwa mmeaminiwa na kuteuliwa kwa sababu ya Imani  ya Tume kuwa mnao uwezo wa kufanya kazi hii, Jambo muhimu mnalotakiwa kulizingatia ni kujiamini na kufanya kazi kwa weledi, na kwamba katika utendaji wa majukumu yenu mnapaswa kuzingatia Katiba ya Nchi, Sheria za Uchaguzi na Kanuni zake, Maadili ya Uchaguzi na Maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume,”alisema Mh. Dkt. Zakia.



No comments