Header Ads

ad

Breaking News

SEKTA ZA UTALII, MISITU NA WANYAMAPORI ZAPAA MWAKA 2023


Na John Mapepele

SEKTA za utalii, misitu na sekta ndogo ya wanyamapori zimeonyesha kufanya vizuri katika kipindi cha mwaka 2023 ukilinganisha na mwaka 2022.

Kwa mujibu wa taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2023 iliyowasilishwa bungeni leo jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Kitila Mkumbo (Mb) inaonyesha kuwa mapato ya utalii yameongezeka kutoka dola za kimarekani kutoka bilioni 2.6 mwaka 2019/2020 hadi kufikia dola za kimarekani dola bilioni 3.4 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 23 ukilinganisha na jitihada za kufikia dola za kimarekani bilioni 6 ifikapo mwaka 2025/2026.

Aidha, mwaka 2023 watalii 1,808,205 walitembelea nchini ikilinganishwa na watalii 1,454,920 mwaka 2022, sawa na ongezeko la asilimia 24.3. Ongezeko hilo limetokana na utangazaji wa utalii, hususan kupitia Programu ya Tanzania -The Royal Tour, kuimarika kwa miundombinu ya utalii ikiwemo barabara na viwanja vya ndege;na utekelezaji wa mkakati wa kuongeza wigo wa mazao ya utalii ikiwemo utalii wa meli na fukwe. Kati ya hao,watalii 888,506 walitembelea Hifadhi za Taifa na watalii 919,699 waliotembelea maeneo mengine ya vivutio vya utalii nchini.

Kwa upande mwingine watalii wa ndani walikuwa 1,985,707 mwaka 2023 ikilinganishwa na watalii 2, 363, 260 mwaka 2022. Kati ya hao watalii 902,176 walitembelea Hifadhi za Taifa mwaka 2023 ikilinganishwa na watalii 787,742 mwaka 2022.

Aidha, mwaka 2023, miche ya miti 35,381 ilioteshwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ikilinganishwa na miche 30, 705,653 iliyooteshwa mwaka 2022. Pia mwaka 2023, jumla ya miche 14,089,944 ilipandwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo misitu ya asili, vyanzo vya maji, makazi na maeneo yaliyoharibiwa kutokana na shughuli za kibinadamu ikilinganishwa na miche 12,473,083 iliyopandwa mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 13.0. Ongezeko hilo linatokana na kampeni na program za upandaji miti zilizofanyika katika maeneo mbalimbali nchini.

Mwaka 2023, mauzo ya bidhaa za misitu nje ya nchi yalikuwa shilingi bilioni 2,0443. Sehemu kubwa ya mapato hayo ilitokana na uuzaji wa zao la unga wa miwati na bidhaa za miwati. Mauzo kutokana na zao la unga wa miwati yalikuwa shilingi bilioni 1,690.82 sawa na asilimia 83 ya mauzo yote. Aidha, bidhaa za miwati zilichangia shilingi bilioni 160.12 na bidhaa nyinginezo zilichangia shilingi bilioni 193 sawa na mchango wa asilimia 8 na asilimia 9 mtawalia.

Mwaka 2023, mapato yatokanayo na sekta ndogo ya wanyamapori yalikuwa shilingi bilioni 634.3 ikilinganishwa na shilingi bilioni 500.5kwa mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 26.7 ongezeko hilo linatokana na juhudi mbalimbali za utangazaji wa vivutio vya utalii ikiwemo program maalum ya Tanzania-The Royal Tour pamoja na uboreshaji wa miundombinu katika maeneo ya Hifadhi.

No comments