NCHIMBI AHITIMISHA ZIARA KWA KISHINDO ARUSHA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi akizungumza na wananchi wa eneo la USA River, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, aliposimama kuwasalimia akiwa njiani kutokea Arusha mjini, akihitimisha ziara ya siku tatu mkoani humo, kisha kuelekea Mji wa Bomang’ombe, Wilaya ya Hai, tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Kilimanjaro.
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Balozi Nchimbi ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Komredi Amos Gabriel Makalla na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Hamid Abdalla.
No comments