Header Ads

ad

Breaking News

KIKWETE ATAJA SIRI YA MAFANIKIO YA MKENGE


Na Omary Mngindo, Bagamoyo

RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete amesema kuwa Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Muharami Mkenge anawapambania wapigakura wake ndio maana maendeleo yanakwenda kwa kasi.

Dkt. Kikwete aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika Mkutano Maalumu ulioandaliwa na Mbunge huyo, uliotoa taarifa ya utekelezaji wa kazi yake katika kipindi cha miaka minne, ukifanyika kwenye ukumbi wa Chuo Cha Sanaa (TASUBA) mjini hapa.

Alisema kuwa pamoja na kwamba Serikali ina mipango mingi ya kimaendeleo kwa wananchi wake, lakini kama Mbunge hatokuwa msumbufu kwa Mawaziri basi maendeleo katika jimboni lake yatasubili sana.

"Mcheza kwao utuzwa msione vinaelea vimeundwa, nampongeza Mbunge wenu Muharami Mkenge kwa namna anavyowapambania wapigakura wake wa Bagamoyo kwani hii ya sasa ni tofauti sana na iliyopita yote ni juhudi zake," alisema Dkt. Kikwete.

Aliongeza kuwa "Mimi nilikuwa Serikali katika nyadhifa mbalimbali pamoja na Urais nimeshuhudia mambo mengi, kama mbunge hutiwasumbua Mawaziri ujue ni vigumu kukufikilia, badala yake wataangaliwa waliokuwa wasumbufu," alisema Dkt. Kikwete.

Akizungumza na na wanaCCM hao, Mkenge alisema kwamba katika kipindi chake cha ubunge wakishirikiana na Mwenyekiti wa Halmashauri Mohamed Usinga, Mkurugenzi Shauri Selenda, Madiwani na watumishi wote wamefanikiwa kuingeza mapato.

"Katika kipindi hicho tumefanikiwa kuongeza mapato kutoka shilingi bilioni 3 mpaka bilioni 5 kwa mwaka, katika mwaka wa fedha wa 2024/2025 halmashauri imepitisha bajeti shilingi bilioni 38.9, kati ya hizo ruzuku kutoka Serikali ya Rais wetu Mama Samia Suluhu ni shilingi bilioni 32.4," 6.4," alisema Mkenge.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete aliwataka wanaBagamoyo kuthamini kai kubwa inayoendelea kutekelezwa na mbunge wao, huku akieleza kuwa Baganiyo ya sasa inaendelea kupiga hatua kubwa ikiwemo ujenzi wa viwanda.

"Niwaambie wananchi wenzangu kabla ya kuanzishwa kwa Halmashauri ya Chalinze wakati huo tulikuwa, lakini katika kipindi hiki tunashuhudia maendeleo makubwa katika nyanja mbalimbali, tuendelee kumuunga mkono mbunge wetu," alisema Ridhiwani.

Mwenyekiti wa CCM mkoani hapa, Mwishee Mlao aliwataka wanachama hao kutulia na kuacha kugawana, huku akiongeza kuwa kila mwanachama ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa wakati wa uchaguzi utakapofika.




No comments