Header Ads

ad

Breaking News

Dkt.Abbasi aiongoza menejimenti kuteta na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

 

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt Hassan Abbasi

Na John Mapepele

MENEJIMENTI ya Wizara ya Maliasili na Utalii ikiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt Hassan Abbasi na Naibu wake Kamishna Benedict Wakulyamba Juni 13 ,2024 wamekutana na Uongozi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi jijini Dodoma.

Mara baada ya kuwasili kwenye ofisi ya wizara, viongozi hao wamepata fursa ya kutambulisha taasisi hiyo mpya na majukumu yake.

Akihitimisha kikao hicho, Dkt. Abbasi ameuhakikishia Uongozi wa Tume kwamba wizara yake ni mdau muhimu wa taasisi hiyo na itashirikiana kikamilifu ili kufikia azma ya Serikali na maelekezo ya Mhe. Rais ya kuzitaka taasisi zote za Serikali kushirikiana na Tume.






No comments