Header Ads

ad

Breaking News

CCM Kibaha yataka madiwani kusoma utekelezaji wa Ilani

Madiwani wakifuatilia taarifa kwenye vishkwambi vyao


Na Omary Mngindo, Mlandizi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kibaha (Kibaha Vijijini) Mkoa wa Pwani, kinewataka madiwani wake kuitisha mikutano itayowasomea utekelezaji wa ilani.

Hayo yamebainishwa na Katibu wa chama hicho wilayani hapa Stiven Shija, katika Baraza la Madiwani mbele ya Mwenyekiti Erasto Makala, Makamu Shomali Minshee na wataalamu, mbalimbali akisema kuwa hatua hiyo inalenga kuwajulisha wananchi kazi zinazofanyika.

"Kila diwani ahakikishe anafanya mikutano katika maeneo yake itayowasomea taarifa za utekelezaji wa kazi zake, ikiwa ni kukisemea chama chetu ambacho ndio chenye ilani inayotekelezwa na viongozi wetu wa Serikali," alisema Shija.

Aidha alozungumzia ujenzi wa Ofisi za chama hicho katika ngazi za matawi, ikiwa ni kuendana na ukubwa wa chama hicho ambacho kinaendelea kuwatumikia wananchi nchini, huku akiwataka wakoheshimishe chama kama anavyokisimamia Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Alisena kuwa anataraji kuwashirikisha wana CCM na wadau mbalimbali katika kulinoresha jengo la chama hicho iliyopo Kitongoji cha kwa Saidi Domo, maarufu Mlandizi bondeni, akisema anataka liwe bora zaidi.

"Tunalo jengo letu lililopo Kitongoji cha kwa Saido Domo, ni jengo zuri lakini itapendeza tukasapoti kazi ambayo umefanyika kwa kushirikiana kuliboresha zaidi, tukiwashirikisha wadau kwa kila mmoja akitupatia alichonacho kwa maana ya vifaa," alisema Shija.

Akizungumzia agizo la madiwani kuitisha mikitano ya kuwasomea wananchi utekekezaji wa Ilani, Mwenyekiti Makala amesema kuwa wamepokea taarifa ya Katibu wao na kwamba watakwenda kufanya hivyo.

"Katibu, sisi madiwani wako tumepokea ushauri uliotupatia kwaniaba yao tunakuhakikishia tunakwenda kufanya mikutano hiyo, ili wananchi waliotuchagua pamoja na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan wapate taarifa za utekelezaji huo, tunatambua kazi kubwa inayotekelezwa na Mwenyekiti wetu wa Taifa," alisema Makala.
Katibu Stiven Shija akizungumza mbele ya Madiwani hao. Picha zote na Omary Mngindo
Madiwani wakifuatilia taarifa kwenye vishkwambi vyao

No comments