Header Ads

ad

Breaking News

Bandari ya Dar es Salaam yatabiriwa makubwa

Na Mwandishi Wetu

WADAU mbalimbali nchini wamepongeza uamuzi wa serikali kuweka washindani wawili wenye uzoefu wa kimataifa kuendesha baadhi ya magati Bandari ya Dar es Salaam wakisema kufanya hivyo mbali ya kuongeza ufanisi utavutia meli nyingi duniani.

Washindani hao wawili ni Kampuni ya Adani International Ports Holding Ltd (AIPH) ambayo ni kampuni tanzu ya Adani Ports and Special Economic Zone Limited (APSEZ) ya India iliyoingia mkataba wa miaka 30 na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuendesha gati namba mbili la makotena (container terminal) bandarini hapo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Mawakala wa Meli (TASAA), Emmanuel Mallya amewaambia waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuweka washindani wawili wenye uzoefu kuendesha magati (terminals) katika Bandari ya Dar es Salaam ni uamuzi wenye afya kwenye uendeshaji wa bandari kwa kuongeza ufanisi na kuvutia biashara zaidi.

“Kazi kubwa ya TPA kama mpangishaji (Landlord) itakuwa kuhakikisha kuwa vigezo muhimu utendaji kazi yaani Key Indicators Performance (KPI) zilizowekwa zinafikiwa. Hata hivyo, Pamoja na maboresho yote ifahamike bandari haiwezi kufikia ufanisi unaotegemewa bila mnyororo mzima wa wadau(total supply chain)kuwa kwenye mezania moja,” amesema Mallya.

Amesema kwa mfano kuhakikisha mizigo inatoka na kuingia bandarini bila kuwepo kwa msongamano mkubwa ni vyema ikafanyiwa kazi kwani itaongeza ufanisi hivyo kuimarishwa barabara na reli ni muhimu kwa maendeleo na ustawi wa bandari.

Ujio wa AIPH unafuatilia kukamilika kwa mikataba mitatu ambayo imeingia Tanzania na DP World Group Oktoba mwaka jana ambapo chini ya makubaliano kampouni hiyo kutoka Dubai itaendesha gati namba nne hadi saba katika Bandari ya Dar es Salaam.

Kwa upande wa ‘documentation’ Mallya ameshauri mifumo (systems) ni vyema iwe inasomana ili mawakala wa meli na forodha, bandari kavuna wengine kwenye mnyororo wapate wepesi wa kufanya documentation ya mizigo yao bila ucheleweshaji kutoka mdau mmoja hadi mwingine kwenye huo mnyororo wa uingizaji na utoaji wa mizigo bandarini.

Wakili Msomi na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya, Dkt Tasco Luambano mbali ya kupongeza kuwepo kwa washindani wawili katika uendeshaji wa shughuli za bandari, amesema mapato ya TPA yataongezeka zaidi.

“Kitachohitajika hapo ni uwazi na ufuatiliaji wa karibu sana utahitajika. Maslahi na usalama wa nchini vizuri ukalindwa kwa gharama yeyote,” alisema Dkt Luambano sambamba na kupongeza hatua mbalimbali zinazofanywa na serilikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Dkt Luambano amesema Bandari ya Dar es Salaam ipo kwenye eneo lenye faida kijiografia kuhuhudumia nchini nyingi zikiwemo za maziwa na kusini ya jangwa la Sahara hivyo ni vizuri bandari ikawa kinara kwa uingizaji na usafirishaji wa mizigo.

Naye Muhamad Nasoro Athaman, mdau na mtumiaji mkubwa wa Bandari ya Dar es Salaam amesema ana matumaini makubwa na waendeshaji wapya kwenye baadhi ya magati kweye bandari hiyo pamoja na mambo mengine itachochea ukuajiaji wa bisahsra ikiwemo uingizaji na usafirishaji wa mizigo.

“Kusafirisha mzigo kwa njia ya Bahari ni salama na wenye uhakika zaidi. Maboresho yanaendelea Bandari ya Dar es Salaam itasaidia bandari yetu kuwa ya ushindani barani Afrika,” alisema Bw Athman na kuongeza ameridhishwa na wasifu wa kiutendaji wa washindani hao wawili.

Kampuni ya East Africa Gateway Limited (EAGL) imekuwa ikifanya kazi kwa ubia na kampuni za AIPH,AD Ports Group na East Harbour Terminals Limited (EHTL) ambapo kampuni ya APSEZ inasimama kama mwanahisa mdhibiti yaani ‘controlling shareholder’.

Kwa mujibu takwimu za TPA zinaonyesha kuwa gati namba 8 hadi 11 zinahusika na ushushaji wa makontena kwa mwaka 2023 pekee ilishusha TEUs 820,000 sawa na asilimia 83 ya mizigo yote kwenye kontana zote banadari hapo.

AIPH imeingia mkataba kuendesha gati namba 8 hadi 11 baada ya iliyokuwa Kampuni ya Tanzania International Container Terminal Services (TICTS) kukoma mkataba wake mwaka 2022 na serikali kutohuishwa tena na hatimaye kuingia mkataba wa miaka ya uendeshaji katika Bandari ya Dar es Saklaam.

No comments