Header Ads

ad

Breaking News

YANGA NAMBA NYINGINE, YAIFURUSHA TABORA UNITED 3-0

Na Mwandishi Wetu

LILE biriani la Yanga, limekuwa tamu, halijatiwa mchanga. Unaweza kusema hivyo baada ya miamba hao kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga mabingwa mara tatu mfululizo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, wamepata mabao yao kupitia kwa Joseph Guede dakika ya 19, bao la pili likifungwa na Maxi Nzengeli dakka ya 49, huku bao la tatu likiwekwa kimiani na Stephane Aziz Ki dakika ya 90.

Kwa matokeo hayo, Yanga wamefikisha pointi 77na kuendelea kubaki kileleni, wakifuatiwa na Azam FC na Simba SC, zote zikiwa zimejikusanyia poniti pointi 66 kila moja.

Kwa upandewa Tabora United, wamebaki na pointi zao 27, wakiwa nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi ya timu 16, baada ya timu zote kwenye ligi Iyo kucheza mechi 29. 

Kwa mujibu wa kanuni za ligi, timu mbili zitashuka daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitapapatuana  na mshindi wa jumla atabaki Ligi Kuu ya NBC.

Timu itakayofungwa itamenyana na timu ya Championship kusaka nafasi ya kusalie Ligi Kuu Bara.

















No comments