Header Ads

ad

Breaking News

WIZARA YA FEDHA YAWANOA WAMILIKI WA MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU KURIPOTI MASUALA YA BAJETI

Mchumi Mkuu Kutoka Idara ya Sera Wizara ya Fedha, Bi. Salome Kingdom, akitoa mada kuhusu Uwasilishaji wa Taarifa za Bajeti kwa Lugha Rahisi, wakati wa kongamano la wadau wa mitandao ya kijamii lililoandaliwa na Wizara ya Fedha mkoani Morogoro. Wadau hao walipata fursa ya kujifunza tafsiri ya viashiria muhimu katika taarifa ya hali ya uchumi na Bajeti ya Serikali, utekelezaji wa bajeti ya Mwaka 2023/24, mafanikio yake na namna mchakato wa uandaaji wa Bajeti unavyofanyika.
 
Asia Singano na Chedaiwe Msuya – WF – Morogoro
SERIKALI kwa kushirikiana na vyombo vya habari meahidi kufanya kazi kwa pamoja hasa katika kipindi hiki cha Bajeti kuelekea uwasilishwaji wa Bajeti Kuu ya Serikali inayotarajiwa kuwasilishwa Bungeni hivi karibuni. 
Hayo yameelezwa na Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi Salome Kingdom, katika Kongamano la Elimu kwa Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii Nchini yaliyofanyika mjini Morogoro katika ukumbi wa mikutano wa NaneNane. 
 
Bi. Salome katika kuwasilisha mada yake kuhusu namna bora ya kuripoti taarifa za bajeti alisema Wizara itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na manufaa yanayopatikana kutokana na ukusanyaji mzuri wa kodi hapa nchini.
 "Serikali inaelekeza zaidi kuongeza mikakati ya ukusanyaji wa mapato ya ndani, hivyo itaendelea kushirikiana na Sekta ya Habari kutoa elimu  kwa wananchi  wasikwepe kulipa kodi," alisema Bi. Salome. 
Aidha, aliwapongeza wadau katika sekta ya habari kwani wana nafasi kubwa katika kuchochea maendeleo ya uchumi wetu kwa njia ya kuwahamasisha wananchi kutekeleza kwa pamoja malengo ya Taifa.
Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Fedha,  Benny Mwaipaja, aliwashukuru wadau na wamiliki wa mitandao ya kijamii nchini kwa kuendelea kufanya kazi bega kwa bega na Wizara  na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo katika kulijenga taifa letu. 
 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Benny Mwaipaja, akizungumza jambo wakati wa Kongamano la Wadau wa Mitandao ya Kijamii ambalo limeandaliwa na Wizara ya Fedha, katika ukumbi wa mikutano wa Nane Nane, mkoani Morogoro, ambapo wadau hao walipata fursa ya kujifunza namna bora ya kuwasilisha Taarifa za Bajeti kwa Lugha Rahisi, Tafsiri ya Viashiria Muhimu katika Taarifa ya Hali ya Uchumi na Bajeti ya Serikali, Utekelezaji wa bajeti ya Mwaka 2023/24, Mafanikio yake na namna Mchakato wa Uandaaji wa Bajeti unavyofanyika.
Wadau wa Mitandao ya Kijamii wakifuatilia Kongamano la Wadau wa Mitandao ya Kijamii lililoandaliwa na Wizara ya Fedha mkoani Morogoro.Wadau hao walijifunza namna bora ya kuwasilisha Taarifa za Bajeti kwa Lugha Rahisi, Tafsiri ya Viashiria Muhimu katika Taarifa ya Hali ya Uchumi na Bajeti ya Serikali, Utekelezaji wa bajeti ya Mwaka 2023/24, Mafanikio yake na namna Mchakato wa Uandaaji wa Bajeti
Mmiliki wa Kvis Media, Khalfan Mlulu, akichangia mada iliyotolewa wakati wa  Kongamano la Wadau wa Mitandao ya Kijamii ambalo liliandaliwa na Wizara ya Fedha mkoani Morogoro. 
Mwenyekiti wa Waandishi wa Mitandao ya Kijamii wanaoandika habari za Wizara ya Fedha, Mathias Canal, akifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa wakati wa  Kongamano la Wadau wa Mitandao ya Kijamii liloandaliwa na Wizara ya Fedha mkoani Morogoro. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Morogoro

No comments