Header Ads

ad

Breaking News

Wahitimu JKT Ruvu waahidi uadilifu

 Wahitimu JKT Ruvu waahidi uadilifu

Na Omary Mngindo, Ruvu

WAHITIMU wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Kambi ya Ruvu Kibaha Mkoa wa Pwani, wameahidi kuwa waadilifu baada ya kumaliza mafunzo yao.

Hayo yamo katika risala yao iliyosomwa na Lulu Godfrey na Julius Mipawa mbele ya mgeni rasmi Nickson John, Mkuu wa wilaya ya Kibaha, katika hafla ya kuhitimishwa kwa mafunzi yao katika kambi hiyo.

"Ndugu mgeni rasmi sisi wahitimu wa mafunzo haya kambi ya Ruvu JKT, tunaahidi kuendelea kuwa waadilifu katika mafunzo yakiwemo tunayotarajia kuyaanza mafunzo stadi," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Akizungumza na wahitimu hao, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha akiwa mgeni rasmi katika mafunzo ya kujitolea Oparesheni miaka 60 ya jeshi hilo, yaliyohudhuliwa na viongozi mbalimbali, alisema akiwa kama kijana mwenzao, wahakikishe wanapokwenda kuanza mafunzo ya ufundi stadi , wahakikishe wanazingatia yale watakayofundishwa," alisema.

"Nikiwa kijana mwenzenu niwaombe baada ya mafunzo haya, mnapokwenda katika ufundi stadi hakikisha unachukua kozi moja itayokuhakikishia kuwa mmoja kati ya wanafunzi 10 bora," alisema Nickson.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa JKT Kanali Robert Kessy alisema kuwa, baada ya mafunzo hayo wahitimu hao wataendelea na mafunzo ya stadi za maisha, yanayolenga kuwapatia walengwa hao ujuzi mbalimbali.

"Baada ya mafunzo haya mnakwenda katika mafunzo ya ufundi stadi yanayolenga kuwapatia ujuzi utaowawezesha kujiajiri pindi mtakapomaliza mkataba wenu wa miaka miwili, hakikisheni mtayazingatia sana" alisema Kanali Kessy.

Naye, Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi, Meja Jenerali Ibrahim Mhona aliwataka wahitimu hao kuyachukua mafunzo hayo kama chakula chao cha kila siku, huku akiwataka waendeleze nidhamu.

"Kwanza nimpongeze Mkuu wa Kikosi hiki Kanali Peter Mnyani akisaidia na maofisa wake kwa kuwapatia mafunzo vijana hawa ambao wameonesha ni namna gani walivyoiva, niwaombe vijana mwendeleze nidhamu mliyokuwa nayo," alisema Meja Jenerali Mhona.

Awali, Mkuu wa Kikosi cha RUVU, Kanali Peter Mnyani kupitia taarifa yake imeeleza kwamba, wahitimu hao wamejifunza masomo mbalimbali ikiwemo silabi, utimamu, usalama wa mwili usomaji wa ramani pamoja na huduma ya kwanza.

"Ndugu mgeni rasmi vijana hawa wamepatiwa ujunzi wa aina mbalimbali ikiwemo masomo ya silabi, usalama wa mwili, usomaji wa ramani sanjali na huduma ya kwanza," ilieleza sehemu ya taarifa.



No comments