Header Ads

ad

Breaking News

UZINDUZI KITUO CHA KUPOZA UMEME IFAKARA MEI 31

Na Mwandishi Wetu

WAKAZI wa Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro wameishukuru na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukamilisha na kuanza kutumika kwa kituo cha kupoza umeme cha Ifakara.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamesema kuwa, zamani walikuwa na changamoto kubwa ya kukatika katika kwa umeme katika eneo hilo hali iliyoathiri shughuli zao za kiuchumi na upatikanaji wa huduma muhimu.

Kituo hicho cha kupoza umeme cha Ifakara kimejengwa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa Ufadhili wa Umoja wa Ulaya ambapo mpaka kukamilika kwake, jumla ya shilingi bilioni 25, zimetumika.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dktt. Doto Mashaka Biteko na Balozi wa Umoja wa Ulaya, Christine Brau wanatarajiwa kuzindua rasmi kituo hicho, Ijumaa Mei 31,2024.




 

No comments