Header Ads

ad

Breaking News

SERIKALI YATENGA SHILINGI BILIONI710 UKARABATI BARABARA ZA WILAYA


Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Zainabu Katimba, amesema serikali inatambua umhimu mkubwa sana wa barabara za wilaya na kusababisha kuongeza bajeti za Barabara za Wilaya (TARURA) kutoka shilingi bilioni 275 hadi shilingi bilioni 710 ili kuhakikisha wananchi wanazifikia huduma mbalimbali kwa urahisi.

Katimba amesema hayo leo Bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Lushoto, Shabani Shekilindi alitakakujua je serikali ina mpango gani wa dharura wa kutengeneza barabara za Maligwi, Wekangwa, Makole na Mbeleyi zilizoathiriwa na mvua ili kurejesha huduma kwa wananchi?

“Serikali inatambua umhimu mkubwa sana wa Barabara za Wilaya na kupelekea kuongeza Bajeti za Barabara za Wilaya (TARURA) kutoka shilingi bilioni 275 hadi shilingi bilioni 710, yote hii ni kuhakikisha miundombinu ya barabara za wilaya inakuwa vizuri na kuwasaidia wananchi kufikia huduma ili waweze kujijenga kiuchumi kupitia shughuli zao za uzalishaji.”

Aidha, Katimba amesema kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ya mara kwa mara na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara, serikali imeanza kutumia teknolojia mbadala katika ujenzi wa Barabara za Wilaya kwa kutumia Mawe ambayo ni gharama nafuu na hudumu kwa muda mrefu zaidi na majaribio yameanza kwenye baadhi ya maeneo ili kuona ufanisi na ubora.

No comments