Header Ads

ad

Breaking News

SERIKALI YA UINGEREZA YAAHIDI KUIPA TANZANIA DOLA MILIONI 3.4

 

Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Selemani Jafo


Na Mwandishi Wetu

SERIKALI ya Uingireza imeahidi kuipa Tanzania dola za Marekani milioni 3.4 kwa ajili ya kufanikisha mkakati wa nishati safi ya kupikia. 


Ahadi hiyo ya Uingereza inakuja zikiwa zimepita siku chache baada ya kinara wa Nishati Safi ya Kupikia Afrika, Rais Samia Sulahu Hassan kuzindua mkakati huo Mei 8, 2024 jijini Dar es Salaam na baadaye kushiriki mkutano wa kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia jijini Paris nchini Ufaransa Mei 14, 2025.

                                     

Kwa kujibu wa mkakati huo inatarajiwa ifikapo 2030 asilimia 80 ya Watanzania watakuwa wanatumia nishati safi ya kupikia.


Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu Dar es Salaam leo, Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Selemani Jafo amesema ahadi ya  Serikali ya Uingereza kuipa Tanzania dola za Marekani milioni 3.4 kwa ajili ya nishati safi ya kupikia nchini ni uthibitisho tosha kwa jitihada za Rais Samia zimeungwa mkono.


Amesema mkutano wa kimataifa wa Nishati safi ya Kupikia uliofanyika nchini Ufaransa umefanikiwa kwa asilimia 100 ambapo dola za Marekani bilioni 2.2 zimekusanywa kupitia wadau mbalimbali walioshiriki.


Waziri Jafo amesema katika mkutano huo hamasa kubwa imetoka kwa Tanzania, kutokana na Mkutano 28 wa Mabadiliko ya Tabianchi ambapo Rais Samia aliileza dunia kuwa ipo haja ya kufanyika mkutano wa nishati safi ya kupikia.


Jafo amesema katika kuhakikisha mkakati wa nishati safi ya kupikia inafanikiwa Tanzania imejipanga ifikapo Januari mwakani 2025 tasisi zote zenye watu kuanzia 300 na kuendelea zihamie na kutumia nishati safi ya kupikia, ambapo katika upande wa taasisi za elimu zimefanya vizuri katika jambo hilo Vyuo vya VETA na Elimu vipo karibu 35 na 30 tayari vinatumia nishati safi ya kupikia.


Amesema Serikali imepanga mkakati wa kila mwaka halmashauri ipande miti milioni 1.5, ambapo kwa halmashauri zote 184 zitakuwa zinapanda miti milioni 276.


Dkt. Jafo amesema mwaka 2022 kwa maelekezo ya Dkt. Samia walitunga kanuni za mwaka 2022 na kuzirejea mwaka jana na muongozo wa kufanya biashara ya Carbon ambapo hadi sasa makampuni 44 yamefanya usajili wa biashara ya Carbon nchini, ambayo imo ya nishati safi ya kupikia .


Mapema Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus amesema Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), imeahidi kutoa dola za Marekani bilioni 2, kwa ajili ya nishati safi ya kupikia kwa kipindi cha miaka 10.


Amesema mafanikio mengine ni pamoja na kutolewa ahadi mbali mbali na washirika wa maendeleo na sekta binafsi ambazo zimeahidi kukusanya dola za Marekani bilioni 2.2 kwa ajili ya nishati safi ya kupikia.


Mkurugenzi huyo amesema mashirika na makampuni 100  yameidhinisha tamko la uongozi wa juu la kuipa kipaombele nishati safi ya kupikia, tamko hilo hasa linadhihirisha nia ya kuchua hatua kwa pamoja na ushirikiano kupitia uzoefu wa upatikanaji wa nishati hiyo.


Katika mkutano huo, ambao Rais Samia alikuwa Makamu Mwenyekiti Mwenza ziliweza kukusanywa hapo hapo dola za Marekani bilioni 2.2 kutokana na nguvu kubwa ya Dkt. Samia katika kuhakikisha Bara la Afrika linatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2030.


Pia, Rais Samia alifanya mazungumzo pembenzoni mwa mkutano huo na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron walitoa tamko la kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya nishati safi ya kupikia, sekta ya maji, uwezeshaji wa wanawake, kilimo, biashara, miundombinu na masuala ya amani na usalama kaskazini mwa Msumbiji na Mashariki ya Congo.


Akigusia malengo ya mkutano huo yameweka kipaombele katika masuala ya nishati safi ya kupikia katika anga za kimataifa, ili kuweza kuchangia fedha kwa ajili ya Bara la Afrika na kutoa ushauri.


Amesema kuwepo kwa sera za nishati safi ya kupikia, kwa vile nchi nyingi bado hazina sera hiyo, ambapo ajenda hasa zilizojadiliwa ni upatikanaji wa fedha za nishati safi ya kupikia barani Afrika na kuharakisha ushirikiano wa wadau mbali mbali kwa vile suala hilo ni pana wanahitaji watu wengi washiriki.


Zuhura amesema Shirika la Kimataifa ya Nishati Duniani (IEA), ambao ndio walioandaa mkutano huo Ufaransa, wamekadiria uwekezaji katika nishati safi ya kupikia ni dola za Marekani bilioni nne zitahitajika kila mwaka, kwa ajili ya Bara za Afrika waweze kuwa na nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2030.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Rais Samia ameifanya Tanzania kuwa kinara wa Nishati safi ya Kupikia, jambo hilo siyo rahisi kwani kila mmoja angelifanya, lakini imekuwa rahisi kwake Dkt. Samia kutokana uwezo wake binafsi, jitihada zake binafsi, utayari wake na mahusiano yake mazuri ya diplomasia kati yake na viongozi wenzake.


Amesema Wizara ya Nishati inaendelea kuweka miundombinu ya upokeaji wa gesi na usambazaji katika makazi pamoja na miundombinu ya umeme ambapo kati ya vijiji 12, 318 wamepeleka umeme na kubakiza vijiji 454, ambavyo vyote vitakamilika ndani ya mwaka huu, ili kufikia azma ya mikakati ifikapo mwaka 2034 watanzania asilimia 80 watumie nishati hiyo.


Naye, Mkuu wa Maendeleo ya Biashara na Ukuaji kutoka M-Gas Resources Ltd, Abdallah Kijangwa amesema wamekuja na suluhisho kwa watanzania wa chini waweze kutumia gesi, hivyo teknolojia yao itamuwezesha mtu kupata huduma ya gesi kwa kuanzia shilingi 1,000 hadi shilingi 10,000 wataweka mita ya kuonyesha matumizi yake.


Mama Lishe wa Kisasa, Eva Francis akitoa ushuhuda wake amesema amepata faida kubwa ya kutumia nishati safi ya kupikia ikiwemo suala la mazingira bora na usafi wa kupika chakula (hakinuki moshi wa kuni), afya za wafanyakazi wake zimeimarika kwa vile hawalalamiki wanaumwa vifua na upatikanaji wa gesi ni rahisi kuliko mkaa na kuni hususani wakati wa mvua zinaponyesha.

 za elimu zimefanya vizuri katika jambo hilo vyuo vya VETA na Elimu vipo karibu 35, lakini 30 tayari vinatumia nishati safi ya kupikia.


Alisema Serikali imepanga  mkakati wa kila mwaka halmashauri ipande miti milioni 1.5, ambapo kwa halmashauri zote 184 zitakuwa zinapanda  miti milioni 276.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam, Mei 17, 2024 kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia uliofanyika Paris Nchini Ufaransa, Mei 14, 2024 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa Kinara na Mwenyekiti Mwenza katika mkutano huo wa kimataifa.

Mama Lishe wa Kisasa, Eva Francis Liboy akizungumzia Faida anazopata kutokana na matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwenye mkutano na Waandishi wa Habari Ikulu jijini Dar es Salaam, Mei 17, 2024

No comments