Header Ads

ad

Breaking News

SEKRETARIETI YA MAADILI, WAHARIRI KUSHIRIKIANA KUTOA ELIMU YA UANDILIFU

Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi akizungumza na wahariri leo Ijumaa Mei 24,2024 jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

KAMISHNA wa Maadili, Jaji Mstaafu, Sivangilwa Mwangesi amevishauri vyombo vya habari vijikite katika kujenga hoja kwa kuchapisha na kutangaza habari linganifu zilizosheheni ukweli bila upendeleo wala uonevu kuhusu maadili ya viongozi wa umma nchini.

 Hayo ameyaeleza leo wakati wa mkutano wake na wahariri wa vvombo mbalimbali vya habari leo Ijumaa Mei 24,2024 jijini Dar es Salaam.

Amesema Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma peke yake haiwezi kutoa elimu ya uadilifu bila msaada wa wadau wengine, wakiwemo wahariri wa vyombo vya Habari, huku akiwataka kwa pamoja kushirikiana kujenga uadilifu nchini kwa kutoa elimu ya maadili na kuibua changamoto zinazokwamisha uadilifu nchini.

"Sekretarieti ya Maadili peke yetu hatuwezi kutoe elimu ya uadilifu, tunahitaji ana msaada wa wadau wengine, wakiwemo wahariri wa vyombo vya Habari, tunaomba tushirikiane kujenga uadilifu nchini kwa kutoa elimu na kuibua changamoto zinazosababisha kukwama kwa maadili," amesema.

Jaji Mstaafu Mwangesi amewataka wahariri kutumia ubunifu wa kalamu zao kuandika habari nyingi zinazoeleza umuhimu wa maadili kwa Viongozi wa Umma nchini. 

"Tuwaondoe viongozi na wananchi hofu tunapotimiza wajibu wetu kwa mujibu wa Sheria na kanuni zilizopo, tusaidiane kukuza uadilifu wa viongozi wetu, kwani uadilifu wa viongozi ukiongezeka utasaidia kukuza maendeleo ya taifa na kuongeza imani ya wananchi kwa Serikali yao," amesema Jaji Mstaafu Mwangesi.

Amesema baada ya mkutano huo, taarifa zinazohusiana na viongozi wa umma zitakazowafikia kwenye madawati yao, wataendelea kuzihoji, kuzidadisi, kuzipembua na kuzichakata kwa mujibu wa Katiba ya nchi, sheria na kanuni zake kabla hawajazitangaza. 

"Mpango uu utaongeza weledi mkubwa na ulinganifu utakaozingatia uhuru wa kujieleza kwa kuzingatia matakwa ya Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995, Kanuni zake na misingi ya taaluma yenu ya Habari," amesema.

Kamishna wa maadili amewapongeze wahariri kwa kazi nzuri wanayoifanya, kazi inayohitaji weledi katika mambo mbalimbali hususan, katika kukuza maadili kwa kuchapisha habari zenye ukweli zikiwemo za uadilifu wa viongozi wa umma, uwajibikaji na wakati mwingine kukosoa baadhi ya mienendo isiyofaa kwa kiongozi wa umma. 

Ameongeza kuwa, kazi hiyo wanaifanya kwa uwezo mkubwa na uzalendo wa hali ya juu, hivyo amelipongeza Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), huku akiushukuru uongozi  wa Jukwaa la Wahariri chini ya Mwenyekiti wake, Deodatus Balile  kwa ushirikiano wao kwa Tume hiyo.

"Mwisho wa Aprili mlikuwa na mkutano wenu Dodoma, nilimsikia Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye akisema nanukuu “Wahariri na waandishi wa vyombo vya habari kwa sasa wanaandika habari bila woga wala hofu kutokana na Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuvifanya vyombo vya habari kuwa huru,” mwisho wa kunukuu. Jamhuri toleo la 7 – 14 Mei, 2024.

Amewaomba wahariri waendelee kutoa habari zinazohusu miendendo ya Viongozi wa Umma, huku akiunga mkono yote yaliyosemwa kwa kuwaasa na kuwaomba wahariri waandike makala za kichambuzi, wafanye mahojiano na wataalamu wa masuala ya maadili pamoja na wananchi, wafanyeni uchunguzi wa kina na kuandika ripoti za kuchambua tabia na maadili ya viongozi kwa kina.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Jane Mihanji, akiuliza swali
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Mhariri Mkuu wa Media Brain,Neville Meena 
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Mtendaji Mkuu wa TEF, wakiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma 
Baadhi ya wahariri wakifuatilia wasilisho la Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu, Sivangilwa Mwangesi
Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu, Sivangilwa Mwangesi

No comments