CHADEMA WATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA KANDA ZOTE
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema
KAMATI kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), iliyokutana kuanzia Mei 11-14 mwaka 2024 Mikocheni jijini Dar es Salaam imekamilisha zoezi la usajili wa wagombea wa nafasi mbalimbali pamoja na kutangaza orodha ya wagombea wake wa Kanda mbali mbali .
1. Usaili na uteuzi wa Wagombea Kanda Nne.
Pamoja na agenda nyingine Kamati Kuu ilipata nafasi ya kuwasaili na kuteua wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika Kanda nne za Magharibi, Nyasa, Serengeti na Victoria kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama.
Kamati Kuu ilifanya uteuzi wa wagombea kwa kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ibara ya 7.7.16(s) Kuteua wagombea wa Uenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Mtunza Hazina wa Kanda.
Aidha, Kamati Kuu iliwaita wagombea wote waliojaza fomu Kwa mujibu wa Kanuni ya 7.2.7 ya Kanuni za Chama ”Waombaji wote wataitwa mbele ya vikao vya Uchujaji kuhojiwa na ama kutakiwa kufafanua taarifa walizozijaza katika fomu zao za maombi.”
Vilevile Kwa mujibu wa Kanuni ya 7.2.13 ya Kanuni za Chama, wagombea ambao ni wajumbe wa Kamati kuu hawakushiriki kuwahoji wagombea wenzao waliokuwa wanagombea nafasi hizo “Wajumbe wa kikao cha uchujaji ambao ni wagombea wa ngazi husika hawatashiriki katika kujadili wagombea wenzao wa nafasi hizo, lakini watashiriki katika kujadili wagombea wa nafasi zingine.”
Wagombea wote ambao hawakuteuliwa watajulishwa sababu za kutoteuliwa kwao kwa mujibu wa Kanuni ya 7.2.8 ya Kanuni za Chama “Vikao vya uteuzi vitatakiwa kuwafahamisha wale wote ambao hawatapendekezwa na kufahamishwa sababu za kutopendelezwa kwao” na wale wote ambao hawataridhika na uamuzi wa Kamati kuu wana haki ya kukata rufaa juu ya uamuzi huo Kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama.
Baada ya mchakato huo wafuatao waliteuliwa na Kamati Kuu.
2. Uchaguzi wa Kanda
Baada ya wagombea kuteuliwa ratiba ya uchaguzi huo utafanyika Mei 29, 2024 katika Kanda za Magharibi, Nyasa, Serengeti na Victoria na utasimamiwa na ofisi ya Katibu Mkuu.
3. Uchaguzi wa Mkoa wa Njombe na Iringa
Kamati Kuu ilipokea na kujadili taarifa za rufaa mbalimbali ikiwemo rufaa za uchaguzi wa Mkoa wa Njombe ambao Kamati Maalum ya Kamati Kuu iliufuta uchaguzi huo kutokana na uchaguzi huo kuendeshwa bila kufuata Katiba na Kanuni za kusimamia chaguzi ndani ya Chama.
Kamati Kuu ilikubaliana na sababu za kufutwa uchaguzi huo na kuagiza ufanyike upya tarehe 25 Mei,2024 na hapatakuwa na uchukuaji wa fomu upya wala usaili bali Wagombea walewale walioshiriki duru ya kwanza ndio watakaogombea.
Aidha, uchaguzi wa Mkoa wa Iringa ambao haukukamilika tarehe 09 Aprili, 2024 utafanyika tarehe 25 Mei, 2025 kwa zile nafasi ambazo hazikukamilisha uchaguzi na Wagombea walewale wa awali ndio Watakaogombea .
Walioteuliwa kugombea nafasi mbalimbali.
KANDA YA SERENGETI
CHAMA
UENYEKITI
1. GIMBI DOTTO MASSABA
2. LUCAS NGOTO NGOTO
UMAKAMU MWENYEKITI
1. JACKSON SCANIA LUYOMBYA
UWEKA HAZINA
1. JACKSON DAUDI TUNGU
2. KHALID SULEIMAN AUSII
3. MAENDELEO BERNARD MAKOYE
4. WILLIAM PIUS SHAYO
BARAZA LA WAZEE
UENYEKITI
1. JACOB RHOBI MONYEKA
2. SYLLVESTER MHOJA KASULUMBAYI
UKATIBU
1. CHARLES BULLET RWEGALULILA
2. KENNEDY MUSA ONYANGO
UWEKA HAZINA
1. MAGDALENA EMMANUEL MKULLA
BARAZA LA WANAWAKE
UENYEKITI
1. BAEGA STEVEN MASUNGA
2. ROSEMARY KASIMBI KIRIGINI
UKATIBU
1. ANGELA DERRICK LIMA
BARAZA LA VIJANA
UENYEKITI
1. BARAKA STEVEN CHARLES
2. MICHAEL EMMANUEL KIHANDA
3. YOHANA ZAKARIA MAGHEMBE
UKATIBU
1. PASCHAL JOSEPH MLAPA
KANDA YA NYASA
CHAMA
UENYEKITI
1. JOSEPH OSMOND MBILINYI
2. PETER SIMON MSIGWA
UMAKAMU MWENYEKITI
1. FRANK GEORGE MWAKAJOKA
2. JOSEPH MWASOTE MJENDA
3. MBEGESE ANOSISYE MWALUPANI
UWEKA HAZINA
1. GERTRUDA JAPHET RENGESELA
2. GRACE RICHARD SHIO
3. REHEMA PAUL MAKOGA
BARAZA LA WAZEE
UENYEKITI
1. CHARLES DAWSON NDENGA
2. HUGHO SAMALI KIMARYO
UMAKAMU MWENYEKITI
1. GERALD SIMALIKE KAJUNI
2. HENRY AMOS MHABUKA
UKATIBU
1. MPONJOLI STANELY MWAIKIMBA
2. SAADAT DAUDI MWAMBUNGU
UWEKA HAZINA
1. LYDIA DONALD MWAIPAJA
BARAZA LA WANAWAKE
UENYEKITI
1. HAPPINESS DAUDI KWILABYA
2. SUZANA CHOGISASI MGONOKULIMA
3. TABIA LUGANO MWAKIKUTI
UKATIBU
1. MARGRETH WILLIAM MLEKWA
UWEKA HAZINA
1. WITNESS MBILILILI MWANI
BARAZA LA VIJANA
UENYEKITI
1. IBRAHIM TUMAINI NYASANGA
2. VICTOR MANENO BALEKE
3. VITUS RUTINWA NKUNA
UKATIBU
1. MAGNUS FIDEL SIMBEYE
UWEKA HAZINA
1. BARAKA ABRAHAMU MWAKIHABA
2. JEREMIAH MAHASILE MNYAMBWA
KANDA YA MAGHARIBI
CHAMA
UENYEKITI
1. DICKSON LUCAS MATATA
2. GASTON SHUNDO GARUBINDI
3. MUSSA DANIEL MARTINE
4. NGASSA GANJA MBOJE
UMAKAMU MWENYEKITI
1. MASANJA MUSSA KATAMBI
2. RHODA EDWARD KUNCHELA
UWEKA HAZINA
1. IDAN LAURENT NDOWA
2. JOSEPHAT CLEMENT SHILOGILE
3. LAURENT MANGWESHI SENGA
BARAZA LA WAZEE
UENYEKITI
1. ADAMU KISINZA MAIGE
2. FRANCIS WILLIAM MSUKA
UMAKAMU MWENYEKITI
1. DONATUS LUPOLE KIPHUNGU
UKATIBU
1. SHABAN RAFAEL MADEDE
2. VENANCE GOMEGWA MWEMELA
BARAZA LA WANAWAKE
UENYEKITI
1. ASHURA MASHAKA MASOUD
2. MARY JAMES MARTIN
3. MONICA TARAMAEL NSARO
UMAKAMU MWENYEKITI
1. REHEMA RAFAEL MWACHA
BARAZA LA VIJANA
UENYEKITI
1. JACKSON FRANK MAULINGE
2. MOHAMED SALUM PUME
UKATIBU
1. IDRISSA KASSIM RUBIBI
UWEKA HAZINA
1. EPIPHANIA ALEX LUTEBUKA
KANDA YA VICTORIA
CHAMA
UENYEKITI
1. EZEKIA DIBOGO WENJE
2. JOHN JUSTINE PAMBALU
UMAKAMU MWENYEKITI
1. BAZIL JUSTINIAN WAZIRI
2. KHALID SWALEHE HUSSEIN
3. MBUTUSYO ALINANINE MWAKIHABA
4. SYLLVESTER MAGELESA MAKANYAGA
UWEKA HAZINA
1. ELIKANA PASCHAL KAHI
2. LEONARD JOSEPHAT MAGERE
3. SIJAONA JAMES KAROLI
BARAZA LA WAZEE
UENYEKITI
1. FABIAN FRANCIS MAHENGE
2. FOCUS EBIGAMBOBYENSI LAURENT
UMAKAMU MWENYEKITI
1. ALPHAXARD NYARUBWA NDIGILE
2. SHIGEMELO JAMES MAKELEMO
UKATIBU
1. GODFREY FAUSTINE MISSANA
2. LOISHIYE LAZARO TEVELI
UWEKA HAZINA
1. PHILIP MUGABU KUGURU
2. SPECIOZA STEPHANO KAMALA
BARAZA LA WANAWAKE
UENYEKITI
1. PASQUINA FERDINAND LUCAS
2. PENDO LUIS NGONYANI
UMAKAMU MWENYEKITI
1. JACQUILINY REVOCATUS KISSANGA
UKATIBU
1. DORICE NICHOLAUS MPATIL
2. ESTHER MUSA FULANO
BARAZA LA VIJANA
UENYEKITI
1. FREDY MICHAEL MASELE
2. SHABAN AVICE MABALA
UKATIBU
1. ALONI ISHENGOMA KILOMBA
Imetolewa leo Ijumaa Mei 17, 2024
John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje
No comments