Header Ads

ad

Breaking News

BENKI CRDB YASAIDIA JITIHADA ZA SERIKALI KUBORESHA MAZINGIRA YA ELIMU

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB imeendelea kusaidia jitihada za Serikali kuboresha mazingira ya elimu nchini, ikiwa ni utekelezaji wa Sera yake ya Uwekezaji kwenye Jamii,  

 
Jitihada hizo zimefanyika mkoani Manyara, katika Wilaya za Mbulu na Babati, siku chache kabla ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB uliofanyika Jumamosi Mei 18, 2024,huku shule zilizonufaika ni Shule za Msingi Shikizi Muungano ya Babati Mjini iliyokabidhiwa madarasa mawili na ofisi ya walimu na shule ya Endagikot ya wilayani Mbulu iliyokabidhiwa darasa na madawati kwa ajili ya watoto wenye uhitaji malumu.

Misaada ya madarasa kwa shuke za msingi Shikizi Muungano yalikabidhiwa na Mkurugenzi wa Manunuzi Benki ya CRDB, Pendason Philemon Mei 14, 2024 na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, ambapo aliishukuru Benki ya CRDB kwa msaada huo unaounga mkono juhudi za serikali kuboresha sekta ya elimu nchini.
 
Mei 15,2024, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Frederick Nshekanabo alikabidhi darasa kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu kwa Shule ya Msingi Endagikot iliyopo wilayani Mbulu na kupokelewa  na Mkuu wa Wilaya wa Manyara, Lazaro Twange,  aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, kwa niaba aliishukuru Benki ya CRDB kwa mara nyingine kuchangia ukuaji elimu katika Mkoa wa Manyara.

"Ujenzi wa madarasa hayo ni sehemu ya utekelezaji wa sera yetu ya uwekezaji kwa Jamii (Policy), inayotenga asilimia moja ya faida ya benki kila mwaka kuwezesha miradi ya maendeleo katika jamii," amesema Nshekanabo.
 
Amesema Benki inatekeleza mradi wa Keti Jifunze unaolenga kutatua changamoto za elimu zinazojumuisha upungufu wa madarasa na ofisi za walimu, madawati, vyoo na miundombinu mingine muhimu.










No comments