Header Ads

ad

Breaking News

YANGA YAIPASUA DODOMA JIJI 2-0, KOMBE LA SHIRIKISHO LA CRDB

Mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize, akiwania mpira wakati wa mechi dhidi ya Dodoma Jiji iliyopigwa Uwanja wa Jamhuri jijini Dododoma, Jumatano Aprili 10,2024. Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MABINGWA wa Ligi Kuu yan NBC na Kombe la Shirikisho la Azam msimu uliopita (sasa Kombe la Shirikisho la CRDB), Yanga, imefanikiwa kusonga mbele hatua ya robo fainali ya mashindano hayo baada ya kuilaza Dodoma Jiji mabao 2-0.

Bao la kwanza la Yanga limefungwa dakika ya tatu ya mchezom, baada ya mpira wa krosi uliopigwa na Augusino Okrah kusukumizwa wavuni na Emmanuel Martin, aliyekuwa akijaribu kuokoa hatari hiyo.

Pamoja na Yanga kutangulia, vijana wa Dodoma Jiji walionesha soka zuri, lakini bahati haikuwa yao, kwani dakika ya 52, walipata penalti, lakini mkwaju uliopigwa na Idd Kipagwile, ulikwenda juu ya lango.

Kwa matokeo hayo, Yanga imetinga hatua ya robo fainali ya mashindano hayo ya CRDB, ikiwaacha watani wao Simba waliopoteza kwa mikwaju ya penalti Mashujaa waliibuka na ushindi wa penalti 6-5 dhidi ya Mashuja ya Kigoma baada ya kufunga bao 1-1 ndani ya dakika 90. 



No comments