Header Ads

ad

Breaking News

YANGA YADHIHIRISHA UKUBWA WAKE, YAIPAPATUA TENA SIMBA

Stephane Aziz Ki, akishangilia bao alilofunga kwa mkwaju wa penalti

Na Frank Balile

WENYE mioyo migumu walikuwepo Uwanja wa Benjamin Mkapa (Lupaso), kushuhudia mechi ya watani wa jadi, Yanga na Simba iliyopigwa leo Jumamosi Aprili 20,2024 jijini Dar es Salaam.

Mashabiki wa Simba wenye mioyo migumu kama alivyowaambia Msemaji wa Klabu hiyo, Ahmed Ally, kuwa wenye mioyo migumu waende uwanjani, lakini wenye mioyo miepesi wasiende, wameshuhudia timu yao ikibanjuliwa mabao 2-1.

Baada ya tambo nyingi zilizotawala jijini Dar es Salaam na nje ya Jiji hili, 'Dabi ya Kariakoo', zimehitimishwa kwa mabingwa watetezi, Yanga, kufanikiwa kuwatungua watani wao Simba mabao 2-1, ushindi ulioendeleza ubabe kwa msimu huu wa 2023/2024.

Katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyopigwa Novemba 5,2023, ilimalizika kwa Yanga kuwagagadua Simba mabao 5-1, ushindi ambao ulikuwa ukiwanyima raha watani hao, hasa baada ya kubandika mabao kwenye barabara kuu yaliyokuwa yakionesha mabao 5-1.

Bao la kwanza la Yanga, ambao wanatetea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC, limefungwa kwa mkwaju wa penalti na  kiungo Stephane Aziz Ki, dakika ya 20. Penalti hiyo ilitokana na makosa ya beki NHussein Kazi, kumchezea vibaya Aziz K ndani ya eneo la hatari.

Bao la pili la miamba hao wa soka limewekwa kimiani na Joseph Guede dakika ya 38, hata hivyo Simba kipindi cha pili iliingia kwa lengo la kutafuta mabao, iliutawala mchezo.

Dakika ya 74, Simba SC walipata bao lililofungwa na Fred Michael, bao lililowapa nguvu za kulisakama lango la wapinzani wao, lakini bahati haikuwa yao.

Kwa ushindi huo, Yanga SC wamefikisha alama 58 wakiendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, huku wakicheza mechi 22, wakifuatiwa na Azam FC yenye alama 51 wakicheza mechi 23, Simba SC wakiendelea kubaki nafasi ya tatu kwa kujikusanyia alama 46, ikicheza mechi 21.











No comments