Header Ads

ad

Breaking News

TCB YAWAJALI WASTAAFU, YAWAPA MIKOPO

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Adam Charles Mihayo, akizungumza katika kikao kazi na wahariri kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.


Na Frank Balile

BENKI ya Biashara Tanzania (TCB), imezidi kuwajali wastaafu waliotiumikia taifa katika nyanja mbalimbali ili waweze kuendesha maisha yao ya uzeeni vizuri, tayati benki hiyo imetoa mikopo kwa wastaafu ambapo hadi sasa imefikia shilingi bilioni 700.

Akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari, Afisa Mtendaji wa Mkuu wa TCB, Adam Charles Mihayo, amesema benki hiyo ndiyo iliyoanzisha mikopo kwa wastaafu, baada ya kuona wanapomaliza muda wao wa kulitumikia taifa, taasisi nyingi za fedha hushindwa kuwakopesha.

Amesema kuwa, hali hiyo ndiyo iliyosababisha Benki ya Biashara ya Taifa (TCB), kuamua kuja na mfumo huo unaowawezesha wastaafu kupata mikopo, huku dhamana ikiwa ni pensheni zao.

"TCB tuliwaangalia wastaafu, hawa wazee wamelitumikia taifa kwa uadilifu sana, hivyo tukaona tuwakumbuke kwa kuwapa mikopo ambayo dhamana yake ni pensheni yake," amesema Mtendaji Mkuu wa TCB.

“Tunafanya utaratibu wa kulipa mishahara wafanyakazi na pia tunatoa mikopo kwa wafanyakazi, hatujawaacha wajasiriamali na makundi mbalimbali,” amesema Mihayo.

Amesema kwa mwaka jana, TCB iliingiza mapato ya shilingi bilioni 184 kutokana na kuaminika na wateja wao, jambo lililochangia kukua kwa amana  ambazo zilifikia asilimia 11.

Mtendaji Mkuu huyo amesema kwa upande wa mikopo inazidi kukua mwaka hadi mwaka, kwa mwaka jana tumefunga na shilingi bilioni 916 sawa na asilimia 9 na mwaka huu mkakati wetu ni kukuza zaidi sekta ya wafanyabiashara na tayari tumetenga shilingi bilioni 300 kwa ajili yao.

Kuhusu mali zao, Mtendaji Mkuu wa TCB amesema mwaka 2023 walifunga shilingi trilioni 1.4, lakini kwa mwaka huu wa 2024 wanakadiria kufunga shilingi trlioni 1.7, huku akiweka wazi kuwa, uwezo huo wanao.

Afisa Habari na Mawasiliano Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri akifafanua jambo katika kikao kazi kilichowakutanisha Benki ya Biashara ya Tanzania (TCB), wahariri na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina
    Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Regina Semakafu, akifafanua jambo kwenye kikao kazi hicho
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Deo Kwiyuka akizungumza katika kikao kazi
Mhariri wa Jamvi la Habari, Hafidh Kido akiuliza swali
Baadhi ya wahariri wakisikiliza kwa makini

No comments