Header Ads

ad

Breaking News

TCB KUTOA MIKOPO YA BILIONI 300

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Adam Charles Mihayo, akiwaeleza wahariri na waandishi wa habari mafanikio ya benki hiyo, leo Jumanne Aprili 9,2024 jijini Dar es Salaam

Na Selemani Msuya 

BENKI ya Biashara Tanzania (TCB), imesema mwaka huu itatoa mikopo ya shilingi bilioni 300 ili kuinua uchumi wa nchi hasa kwa wajasiriamali.

Hayo yamesemwa leo Aprili 9,2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TCB, Adam Mihayo, wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari Dar es Salaam, ikiwa ni mwendelezo wa mikutano ya taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Mihayo amesema benki hiyo ambayo mwakani inafikisha miaka 100 tangu kuanzishwa mwaka 1925, imepitia mengi inagawa sasa inaendelea vizuri na pamoja na mikopo hiyo, imedhamiria ndani ya miaka mitatu kushika nafasi ya tatu kwenye taasisi za fedha nchini.

Amesema TCB inahudumia Watanzania wa makundi zaidi ya milioni mbili, hivyo ili kufanikisha lengo la kukua kibiashara na huduma, mwaka huu itatoa mikopo ya Sh bilioni 300 kwa wafanyabiashara na wajasiriamali 2,000.

“TCB tumejipanga kuchangia ukuaji uchumi na biashara kwa kufikia watu wengi hasa wajasiriamali. Lakini pia tunarajia faida ya benki yetu kabla ya kodi itaongezeka hadi Sh bilioni 40 na hilo limeoineka kwani katika robo ya kwanza ya mwaka 2024 tumepata faida ya zaidi ya Sh bilioni 10 kutoka Sh bilioni 3 robo ya kwanza ya mwaka 2023,” amesema.

Amesema dhamira ya TCB kuwa benki namba tatu kwa ukubwa nchini, itafanikiwa kwani inafikia watu wengi wanaohitaji huduma za kibenki, hivyo kuomba Watanzania kuitumia ili kunufaika kiuchumi.

Mihayo amesema hadi sasa TCB ina matawi 82, ATM 1,031, wakala 6,000 ikiwa ni ongezeko la wakala 4,416 na mipango yao ni kuongeza wakala hadi 10,000 na huduma zao zimejiunga na Mkoba.

Afisa Mtendaji Mkuu huyo amesema robo ya mwaka jana benki ilitoa mikopo inayofikia Sh bilioni 852 na mwaka huu wametoa Sh bilioni 983 likiwa ni ongezeko la asilimia 15.4, huku ikiwa imeajiri zaidi ya wafanyakazi 1,080.

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Regina Semakafu akifafanua jambo katika kikao kazi
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Deo Kwiyuka akizungumza katika kikao kazi kati ya maofisa wa benki hiyo, wahariri na waandishi wa habari leo Jumanne Aprili 9,2024 jijini Dar es Salaam
Afisa Habari na Mawasiliano Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kusuri akifafanua jambo katika kikao kazi kilichowakutanisha Benki ya Biashara ya Tanzania (TCB), wahariri na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina
Wahariri wakisikiliza wasilisho lililokuwa likitolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Adam Charles Mihayo (hayupo pichani)
Wahariri na waandishi wa habari wakiwa makini kusikiliza wasilisho.

No comments