Header Ads

ad

Breaking News

TAEC YAZIDI KUWALINDA WANANCHI, YASIMAMIA UDHIBITI MATUMIZI SALAMA YA MIONZI

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Profesa Lazaro Busagala, akifafanua wasilisho lake katika kikao kazi kilichofanyika leo Jumatatu Aprili 29,2024 jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Sluhu Hassan imeendelea na juhudi za kusimamia udhibiti wa matumizi salama ya mionzi ili kuepuka madhara yake.

Akizungumza katika kikao kazi kilichosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Profesa Lazaro Busagala, amesema hadi mwaka 2022/2023 jumla kaguzi 971 kwa mwaka zilifanyika ukilinganisha na kaguzi 244 kwa mwaka 2016/2017. 

Profesa Busagala amesema hilo ni ongezeko la asilimia 298, ambazo ni kaguzi nyingi kuliko viwango vya kimataifa vinavyotakiwa.

Kikao kazi hicho kiliwashirikisha waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari, ambapo TAEC walikuwa wakielezea kazi na mafanikio yao, huku wakieleza udhibiti matumizi salama ya mionzi jinsi serikali ilivyofanikiwa kuongeza idadi ya wale wanaopewa lesseni kwa asilimia 102 yaani kutoka lesseni 297 kwa 2016/2017 hadi wastani wa 767 kwa mwaka.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kuwa, sababu kubwa ya matokeo hayo ni ongezeko la juhudi za udhibiti ikiwemo kufanya kaguzi za mara kwa mara, kufungua ofisi mbalimbali na kutumia mifumo ya TEHAMA.

"Katika utekelezaji wa Sheria ya Nguvu za Atomu Na. 7 ya 2003, Serikali imefanikiwa kusajili wataalam wa mionzi 788 wenye sifa za kutoa huduma ya mionzi kwa watu, ambapo ndani ya miaka mitatu imesajili wataalum 1,289 wa kutoa huduma ya mionzi kwa wagonjwa, kutengeneza, kukarabati na kuendesha vifaa vya nyuklia. Jambo hili lilikuwa halifanyiki kwa kipindi cha nyuma," amesema Profesa Kusagala.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita kupitia TAEC imeendelea na juhudi za kuhamasisha matumizi salama ya teknolojia ya nyukilia nchini, ambapo juhudi kubwa kuhakikisha wananchi wanaelewa fursa zilizopo katika matumizi salama ya sayansi ya nyuklia kwa ajili ya kujilitea maendeleo.

Profesa Busagala amesema kuwa, TAEC imeongeza program za kujitangaza kutoka 12 hadi 60 kwenye televisheni, redio, magazeti, mitandao ya kijamii na kushiriki katika maonesho mbalimbali.

Ameongeza kuwa, vifaa vya kisayansi ni nguzo muhimu katika kudhibiti athari za mionzi, tafiti, usimamizi na uendelezaji wa Teknolojia ya Nyuklia, ambapo Serikali ya Awamu ya Sita, inaendelea kuweka bajeti na kununua vifaa, ambapo vifaa vya jumla ya shilingi bilioni 2.9  vinaendelea kununuliwa.

"Serikali ya Awamu ya Sita imefanikiwa kuongeza tengeo la bajeti ya utafiti kwa TAEC hadi kufikia shilingi milioni 450 katika mwaka wa fedha 2023/2024, juhudi hizo zimefanyika ili kupata fursa zaidi za sayansi na teknolojia ya nyukilia na pia kuwalinda wananchi na mazingira dhidi ya madhara ya mionzi.

Mkurugenzi Mkuu huyi amesema katika miaka mitatu machapisho 25 ya kitafiti yamepatikana katika juhudi hizo.

Afisa Habari na Mawasiliano Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kusuri akizungumza katika kikao kazi.
Watendaji wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), wakisikiliza maswali kutoka kwa wahariri na waandishi wa habari.
Wahariri na waandishi wa habari akifuatilia wasilisho.
Wahariri na waandishi wakiwa makini kusikiliza
Wahariri wakiwa makini kusikiliza
Wahariri wasikiliza

No comments