Header Ads

ad

Breaking News

TAEC YAPATA MAFANIKIO, MADUHULI YA SERIKALI YAFIKIA SHILINGI BILIONI 10.9

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Profesa Lazaro Busagala, akifafanua wasilisho lake katika kikao kazi kilichofanyika leo Jumatatu Aprili 29,2024 jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Profesa Lazaro Busagala amesema makusanyo ya maduhuli ya serikali yameongezeka kutoka shilingi bilioni 8.7 mwaka wa fedha 2020/2021 hadi shilingi bilioni 10.9 bilioni kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Aprili 29,2024 jijini Dar es Salaam na Profesa Busagala katika kikao kazi kati ya wahariri na waandishi wa vyombo vya habari mbalimbali, ambapo amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita kufungua ofisi za kanda, mipakani na kutumia mifumo ya TEHAMA kama vile TANCIS, TeSWS na EDMS katika kutoa huduma.

"Mafanikio haya yametokana na juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kufungua ofisi za kanda, mipakani na kutumia mifumo ya TEHAMA kama TANCIS, TeSWS na EDMS katika kutoa huduma.

Kuhusu uboreshaji wa mazingira ya kufanya biashara, Mkurugenzi Mkuu huyo amesema wamefanikiwa kupunguza siku za utoaji wa cheti cha uchunguzi wa mionzi (RAC) kutoka zaidi ya siku saba hadi kufikia wastani wa saa tatu hadi siku moja kwa asilimia 98.

Amesema awali utaratibu wa RAC ulikuwa una mlolongo mrefu ambao ulisababisha malalamiko mengi kutoka kwa wadau mbalimbali, lakini kwasasa mfumo wa kielektronic: rac.taec.go.tz umesaidia sana.

Profesa Busagala amesemam kuwa, Serikali ya awamu ya sita imeondoa tozo na kupunguza tozo kwa kuamua kubeba gharama za upimaji (subsidy), hasa kwa wanaosafirisha bidhaa nje ya nchi kwa kupunguza kutoka asilimia 0.2 ya malipwani kuwa asilimia 0.1 ya malipwani, sawa na punguzo la asilimia 50.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema wafanyabiashara wadogo hupatiwa huduma ya upimaji wa sampuli bure sawa na punguzo la asilimia 100, huku wakiboresha matumizi ya TEHAMA ambayo yamesaidia kufanikisha mambo mengi, ikiwemo kuunganisha mifumo ya TAEC (EDMS), ifanye kazi kwa pamoja na ile mingine ya serikali mfano GePG, TANCIS, TeSWS yamekuza mawasiliano ndani na nje ya TAEC na kuleta matokeo chanya katika maeneo mbalimbali.

Kuhusu rasilimali watu, Prpfesa Busagala amesema kwamba, Serikali ya Awamu ya Sita imeongeza idadi ya watumishi wa kudumu kutoka 89 hadi kufikia 142, jambo lililosaidia TAEC kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuwahudumia wananchi kwa uharaka zaidi.

"Serikali imetatua tatizo la watumishi wa TAEC kupandishwa vyeo, tatizo lililodumu kwa muda mrefu. Watumishi 57 wa TAEC walikuwa na matatizo yaliyodumu kwa muda mrefu lakini Serikali ya awamu ya sita imeyatatua," amesema Profesa Busagala.

Amesema Serikali kupitia TAEC ipo katika hatua za mwisho za kukamalisha mpango wa ufadhili kwa vijana wa kitanzania kusoma vyuo vya nje ya nchi masomo ya teknolojia na sayansi ya nyuklia katika ngazi ya shahada za uzamili, ambapo kila mwaka vijana watanzania watano watapata ufadhili huu.

Profesa Busagala amesema lengo la ufadhili huo ni kuongeza idadi ya wataalam nchini katika nyanja ya teknolojia na sayansi ya nyuklia ili kuhakikisha nchi inanufaika ipasavyo na fursa za sayansi ya nyuklia.

 "Serikali ya Awamu ya Sita kupitia TAEC imewajengea uwezo wa kitaalam watumishi ili kujenga taifa lenye uwezo katika teknolojia ya nyuklia, TAEC imeshasomesha watumishi 29 na na inaendelea kusomesha wengine 32 ndani ya miaka mitatu, jumla itakuwa watumishi 61, mpango huu ni muhimu kwa ustawi wa taifa letu katika sekta ya sayansi na teknolojia ya nyuklia," amesema.

 Amesema Serikali kupitia TAEC, imebuni na kutengeneza trela maalum la kubebea vyanzo vya mionzi, awali, watumishi na vyanzo vya mionzi walikuwa wanakaa kwenye gari moja linalotenganishwa na vifaa ambavyo havizuii ipasavyo mionzi.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa, jambo hilo lilikuwa linahatarisha usalama wa watumishi wanaosafirisha vyanzo vya mionzi, wananchi  na mazingira kwa ujumla.

Kuhusu bajeti, Profesa Busagala amesema Serikali imefanikiwa kuongeza tengeo la bajeti ya utafiti kwa TAEC hadi kufikia shilingi nilioni 450 katika mwaka wa fedha 2023/2024, ambapo juhudi hizo zimefanyika ili kupata fursa zaidi za sayansi na teknolojia ya nyukilia na pia kuwalinda wananchi na mazingira dhidi ya madhara ya mionzi.

Profesa Busagala amesema katika miaka mitatu, machapisho 25 ya kitafiti yamepatikana, huku akisisitiza kwamba Serikali imeendelea  na juhudi za kusimamia udhibiti wa matumizi salama ya mionzi ili kuepuka madhara yake.

Amesema hadi mwaka 2022/2023 jumla kaguzi 971 kwa mwaka zilifanyika ukilinganisha na kaguzi 244 kwa mwaka 2016/2017, hiyo ni ongezeko la asilimia 298, kaguzi hizi ni nyingi kuliko viwango vya kimataifa vinavyotakiwa.

Katika kudhibiti matumizi salama ya mionzi, Serikali ilifanikiwa kuongeza idadi ya wale wanaopewa lesseni kwa asilimia 102 kutoka leseni 297 kwa 2016/2017 hadi wastani wa 767 kwa mwaka, sababu kubwa ya matokeo hayo ni ongezeko la juhudi za udhibiti ikiwemo kufanya kaguzi za mara kwa mara, kufungua ofisi mbalimbali na kutumia mifumo ya TEHAMA. 

Katika utekelezaji wa Sheria ya Nguvu za Atomu Na. 7 ya 2003, Serikali imefanikiwa kusajili wataalam wa mionzi 788 wenye sifa za kutoa huduma ya mionzi kwa watu, ambapo ndani ya miaka mitatu, imesajili wataalum 1,289 wa kutoa huduma ya mionzi kwa wagonjwa, kutengeneza, kukarabati na kuendesha vifaa vya nyuklia, awali jambo hilo lilikuwa halifanyiki.

Afisa Habari na Mawasiliano Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kusuri akizungumza katika kikao kazi.

Wahariri na waandishi wa habari wakifuatilia wasilisho

Wakiwa makini kusikiliza wasilisho
Wakifuatilia wasilisho
                                                Wahariri na waandishi wakifuatilia wasilisho
Wahariri wakiwa makini kusikiliza wasilisho

No comments