Header Ads

ad

Breaking News

RIDHIWANI MGENI RASMI NGUMI MSATA

Diwani wa Kata ya Msata, Selestine Semiono

Na Omary Mngindo, Chalinze

NAIBU Waziri wa Utumishi Ridhiwani Kikwete kesho Aprili 12,2024 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa ngumi utaopigwa kwenye ukumbi wa Faida uliopo Msata.

Ngumi hizo zitazotanguliwa na pambano la awali litalowakutanisha madiwani Selestine Semiono wa Msata na Nassa Karama wa Bwilingu, limedhaminiwa na Mussa Ndyamukama na Big Fashion ya Msata.

Wakizungumza kuelekea pambano la utangulizi litakalowakutanisha mabondia kutoka Bagamoyo, Kiwangwa na Msata, Semiono na Karama wamejiganga kuelekea pambano hilo litakalokuwa na kiingilio cha sh.5,000, huku jukwaa kuu wakilipa zaidi.

"Nimejiandaa vizuri kwa ajili ya pambano hili na nina uhakika nitamchakaza Nassa, nimefanya mazoezi ya kutosha, lakini nasikitika kwani Mkurugenzi Ramadhani Possi atalazimika kuitisha uchaguzi mdogo, Nassa hatotoka ulingoni salama," alisema Semiono.

Naye Nassa alisema kuwa, mpambano huo wa utangulizi atautumia kama kisasi, kutokana na wao kuishi pamoja kwa miaka mingi, huku wakiwa na mapambano ya hapa na pale katikataa wao.

"Niwahakikishie wanahabari, siku hiyo Semiono sitampa nafasi ya kuutawala ulingo, nitampiga kipigo ambacho hatakisahau, nimejiandaa vizuri, nina mashaka ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo," alisema Nassa.

Akizungumzia pambano hilo, Ndyamukama alisema maandalizi yamekamilika, huku akimshukuru Mbunge Ridhiwani na Diwani Semiono kwa juhudi zao za kuendeleza michezo katika kata hiyo.

"Mbunge wetu Ridhiwani Kikwete amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha michezo, hivi karibuni alikabidhi jezi kwa timu yetu iliyoshiriki Ligi ya Wilaya, pia Diwani Semiono anapigania michezo," alimalizia Ndyamukama.

Diwani wa Kata ya Bwiligu, Nassa Karama
Mdhamini wa pambano, Mussa Ndyamukama

No comments