Header Ads

ad

Breaking News

RAIS WA ZANZIBAR DKT.MWINYI AONGOZA WANANCHI MAZIKO YA MBUNGE WA JIMBO LA KWAHANI

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akibeba jeneza likiwa na mwili wa marehemu Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar, Ahmada Yahya Abdulwakil, katika Msikiti wa Mpendae kwa ajili ya Ibada ya Sala ya Maiti iliyofanyika katika Msikiti huo leo 9-4-2024 na kuzikwa Kijijini kwa Muyuni C Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali na Wananchi katika Sala ya Maiti, kumsalia Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Marehemu, Ahmada Yahya Abdulwakil aliyefariki jana na kuzikwa leo Kijijini kwao Muyuni C Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja leo 9-4-2024.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na viongozi mbalimbali na wananchi katika kuitikia dua ikisomwa na msaidizi wa Imamu wa Msikiti wa Mtoro Dar es Salaam, Sheikh Abdalla Mundhiri, baada ya kumalizika kwa sala ya maiti, kumsalia Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar, Ahmada Yahya Abdulwakil iliyofanyika katika Msikiti wa Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja leo 9-4-2024, aliyefariki jana na kuzikwa leo kijijini kwao Muyuni C Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar, Ahmada Yahya Abdulwakil, aliyefariki jana na kuzikwa leo Kijijini kwao Muyuni C Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja leo 9-4-2024. (Picha zote na Ikulu)

No comments