Header Ads

ad

Breaking News

RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 30 TANGU KUTOKEA MAUAJI YA KIMBARI NCHINI RWANMDA


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan akielekea kwenye eneo la makaburi kwa ajili ya kuweka shada la maua wakati wa maadhimisho ya miaka 30 tangu kutokea mauaji ya Kimbari Kigali nchini Rwanda. Maadhimisho hayo ya miaka 30 yamefanyika katika Makumbusho ya Mauaji ya Kimbari, Kigali nchini Rwanda na kuhudhuriwa na viongozi kutoka nchi mbalimbali, Aprili 7, 2024.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima mara baada ya kuweka shada la maua kwenye eneo la makaburi ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari Kigali nchini Rwanda, Aprili 7, 2024. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakimshuhudia Rais wa Rwanda, Paul Kagame akiwasha mwenge wakati wa kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari Kigali nchini Rwanda, Aprili 7, 2024.

No comments