Header Ads

ad

Breaking News

MSAJILI HAZINA AFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA KAMPUNI YA PERSEUS YA AUSTRALIA


Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, Aprili 20, 2024 amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Perseus ya nchini Australia iliyowakilishwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Jeff Quartermaine na Afisa Fedha Mkuu wa kampuni hiyo, Lee Anne de Bruin.

Kampuni ya PERSEUS imenunua hisa za Kampuni ya ORECORP iliyokuwa inamiliki mgodi wa Nyanzaga uliopo Geita.

Kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma, pamoja na mambo mengine, Perseus imekubali kuongeza asilimia 4 ya hisa za Serikali "Free Carried Interests" na kuifanya Serikali ya Tanzania kumiliki asilimia 20 ya mgodi huo kutoka asilimia 16 za awali.



No comments