Header Ads

ad

Breaking News

MOROGORO YANUFAIKA NA ZAO LA KARAFUU

Na Mwandishi Wetu Morogoro

KATIKA msimu wa 2023 Mkoa wa Morogoro umefanikiwa kuzalisha tani 2,000 za karafuu zenye thamani ya shilingi bilioni 36.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa mkoa huo, Dk Musa Ally Musa, wakati wa akizungumza na wadau wa mazao ya viungo, ambapo ameweka bayana kuwa tani hizo 2,000 zimezalishwa katika Halmashauri ya Morogoro pekee, lakini aliongeza kwamba umaarufu wa zao hilo unazidi kuongezeka katika mkoa huo.

“Hali ya hewa na ardhi yenye rutuba inatoa fursa ya kuzalisha mazao ya viungo kwa tija na kwa kukidhi viwango vya kimataifa ambapo mazao ya viungo tunayoyawekea mkazo hivi sasa ni karafuu, mdalasini (cinnamon), iliki (cardamom), na mchaimchai (lemongrass),” amesema.

Amesema zao la karafuu linapenda sehemu zenye miinuko na mkoa wa morogoro una sehumu nyingi za aina hiyo, hivyo kuwatawa wakulima kuchangamkia fursa hiyo ambayo ina soko la uhakika.

Mussa amesema ulimaji wa zao hilo umeanza kuimarika katika Wilaya za Morogoro Vijijini, Kilombero na Mvomero na katika Halimshauri ya Wilaya ya Mlimba.

Mbali ya Mkoa wa Morogoro, jitihada inafanywa ili kilimo cha karafuu kiimarishwe katika Mkoa wa Tanga na mkoa wa Pwani, hali ya hewa ni sawa na ile ya Zanzibar.

Zanzibar pekee inazalisha tani 4,000 za karafuu na Zanzibar ni maarufu katika uzalishiji wa karafuu duniani. Morogoro tayari inazalisha nusu ya karafuu yote inayozaliwa Zanzibar. Hii maana yake ni kwamba kuna uwezekano wa Tanzania kuzalisha tani 8,000 ifikapo 2026 kama mikoa ya Morogoro na Tanga itazalisha jumla ya tani 4,000 ifikapo mwaka huo.

Ulimaji wa karafuu Bara umetokana utafiti na ushauri wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Kusin mwa Tanzania (SAGCOT), taasisi inayowashirikisha wadau katika sekta binfasi katika kulima mazao na kuendeleza minyororo ya thamani ya mazao hayo.


No comments