M-BET YAMZAWADIA MSHINDI WA PERFECT 12 MILIONI 140.5, YAZINDUA KAMPENI YA M-BET LIKES YOU
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-Bet Tanzania,Allen Mushi (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi, mshindi wa droo ya Perfect 12, Yahya Bakari ambaye ameshinda sh.milioni 140.5.Katika hafla ya makabidhiano hayo, M-bet pia ilizindua kampeni mpya ijulikanyo kwa jina la M-Bet Likes You ambayo itawawezesha washindi mbalimbali kushinda zawadi ya kushuhudia mchezo wa fainali wa mataifa ya Ulaya nchini Ujerumani kuanzia Juni 14 mpaka Julai 14.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHABIKI wa klabu ya Simba na Arsenal, Yahya Saidi
Bakari ameshinda sh 140,503,890 baada ya
kubashiri kwa usahihi matokeo ya ligi mbalimbali duniani kupitia mchezo wa Perfect 12 wa kampuni M-Bet Tanzania.
M-Bet Yazindua Kampeni Mpya
Mbali ya
kumzawadia mshindi huyo, M-Bet pia imezindua kampeni mpya ijulikanyo kwa jina la M-Bet Likes You
ambayo itawawezesha washindi mbalimbali
kushinda zawadi ya kushuhudia mchezo wa fainali wa mataifa ya Ulaya nchini
Ujerumani kuanzia Juni 14 mpaka Julai 14.
Maoni ya Mshindi
Bakari ambaye ni
mkazi wa mkoa wa Singida alisema kuwa amefurahi kutwaa kitita kikubwa cha fedha
ambapo katika maisha yake hakuwa na mategemeo ya kukipata.
Alisema kuwa yeye ni mfanyabiashara mdogo na ushindi huo utamfanya kuongeza mtaji na kuwasomesha watoto wake.
“Mimi ni mfanyabiashara au wakala wa huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu. Sikuwa na mtaji mkubwa, kupitia fedha ya M-Bet, nitawezza kukuza mtaji na vile vile kusomesha watoto wangu,” alisema Bakari.
Alisema kuwa
ushindi wake haukuwa rahisi kwani alipitia ugumu hasa kubashiri matokeo ya
mechi kati ya Chelsea na Manchester United ambapo Chelsea iliibuka mshindi wa
mabao 4-3 katika dakika za mwisho.
“Sikuweza
kuangalia mechi hiyo ambapo nilimpa ushindi Chelsea kwa sababu ilikuwa inacheza
nyumbani. Nilipokuwa natembea, nikaambiwa kuwa Machester United inaongoza na ni
dakika za nyongeza, nikaamini kuwa nimekosa mkeka huo tena kwa mechi moja tu,
niliporejea kuangalia matokeo, nikaona Chelsea wameshinda, nilifurahi sana
kwani hapo nikajua kuwa sasa mimi ni miongoni mwa washindi,” alisema.
M-Bet Kutoa Zawadi Zaidi
Kwa upande wake,
Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi alimpongeza Bakari kwa kuwa miongoni
mwa mamilionea na kuwaomba Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 kujarbu
bahati yao kwa kubashiri na M-Bet.
Kampeni ya M-Bet Likes You
Mushi alisema
kuwa M-Bet imedhihirisha kuwa ni nyumba ya washindi na mamilionea kwani mpaka
sasa Watanzania kadhaa wameshindia fedha nyingi kupitia michezo yao ya
kubashiri.
Wakati huo, Kampuni hiyo imezidua kampeni mpya ijulikanayo kwa jina la M-Bet Likes You ambapo zawadi kubwa ni kushinda tiketi ya kushuhudia fainali ya michuano ya Mataifa ya Ulaya iliyopangwa kuanza Juni 14 na kumalizika Julai 14 nchini Ujerumani.
Mushi alisema kuwa washiriki wanatakiwa kubashiri na M-Bet ambapo mashabiki wa soka ambao watapata likes kuanzia 1,000 watajishindia safari ya Ujerumani ambayo itagharimiwa na kampunii yao.
Alifafanua kuwa
kampeni hiyo haina idadi ya washindi kwani hata wakifika 1,000, watakwenda
kushuhudia mechi ya fainali tena kwa kukaa jukwaa la karibu na uwanja.
Mshindi wa droo ya Perfect 12, Yahya Bakari akinyoshea kidole eneo lililoandiwa kiasi cha sh. milioni 140.5 alizoshinda kupitia droo ya Perfect 12 ya kampuni ya M-Bet. Mbali ya makabidhiano hayo, M-Bet pia ilizindua kampeni mpya ijulikanyo kwa jina la M-Bet Likes You ambayo itawawezesha washindi mbalimbali kushinda zawadi ya kushuhudia mchezo wa fainali wa mataifa ya Ulaya nchini Ujerumani
No comments