Header Ads

ad

Breaking News

KULIIBIA TAIFA NI KUJIIBIA MWENYEWE - BALOZI DKT. NCHIMBI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akimsikiliza mmoja wa wananchi katika ziara yake

Na Mwandishi Wetu, Njombe
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amekemea tabia ya wizi na kulaani vikali watu wote wenye tabia ya wizi na vitendo vya rushwa.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa stendi ya zamani ya makambako mkoani Njombe, Balozi Dkt. Nchimbi amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa na kukemea tabia ya vijana kutofanya kazi na badala yake kujikita kwenye tabia za kufanya kazi zisizo halali.

Akitoa majibu ya kero za wananchi kuhusiana na tabia ya wizi na ujangili, Balozi Dkt. Nchimbi amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ndug. Mtaka kufanya uchunguzi ili kubaini vinara wa ujambazi na mauaji kwa lengo la kuthibiti kabisa tabia hizo.

Aidha, Balozi Dkt. Nchimbi amewataka viongozi wote wa serikali kuwa na matumizi sahihi ya fedha za umma na kuwataka TAKUKURU kuendelea na kazi yao nzuri ya kufuatilia miradi yote ya kimaendeleo kuanzia inavyoanza hadi kukamilika kwake.

" TAKUKURU hakikisheni miradi yote hasa mikubwa ya maendeleo mnaifuatilia tangu ikiwa inaanza kuhakikisha hakuna fedha ya umma inaibiwa na kutumika vibaya, tunataka thamani ya fedha ieandane na thamani ya mradi husika,"alisema.

Katibu Mkuu huyo wa CCM amewataka viongozi wa serikali mkoani Njombe kuzitumia vizuri fedha za maendeleo zilizoletwa mkoani humo.

"Mkoa wa Njombe mmepata shilingi bilioni 900, fedha hizo ni nyingi sana, nitumie nafasi hii kuwapongeza Mkuu wa mkoa na wabunge wenu kwa kutengeneza ushawishi wa kumfanya Rais Dkt. Samia kutoa fdha hizo ndani ya mkoa wenu," alisema na kuongeza.

"Vyombo vyote vya serikali vyenye mamlaka ya matumizi ya fedha za miradi hakikisheni pesa hizo zinatumika kihalali na msisubiri kukamata walioiba bali ni lazima mdhibiti na kuzuia mianya ya uibaji."
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akinong'onezwa jambo na mwananchi mmoja katika ziara yake
Katibu wa NEC-Oganaizesheni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Issa Haji Gavu akihutubia katika mkutano wa hadhara Makambako mkoani Njombe

No comments