Header Ads

ad

Breaking News

CCM BAGAMOYO YATAKA BARABARA YA MAKOFIA-MLANDIZI KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI

Wajumbe wa Kamati ya Siasa wakiangalia taarifa ya mradi  waliotembelea wilayani hapa.


Na Omary Mngindo, Bagamoyo

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, kimeitaka Wakala wa Barabara nchini TANROAD'S kuijenga kwa kiwango cha lami kwa awamu barabara ya Makofia, Mlandizi.

Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa chama hicho wilayani hapa Alhaj Abdul Sharifu, mbele ya Kamati ya Siasa ya chama hicho, wakiwa eneo la Maliasili njiapanda ya Magereza Msata, akiunga mkono hoja ya Mohamed Usinga Diwani wa Yombo.

Kauli huyo imetanguliwa na taarifa fupi kutoka kwa Mhandisi Emmanuel Mwakyusa kutoka TANROAD'S Pwani, aliyeelezea mipango ya ujenzi wa barabara Bagamoyo Saadan Tanga, ambayo ujenzi wake umeanzia Tanga kuja Bagamoyo.

Aboubakary Mlaw,a Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilayani Bagamoyo alizungumzia changamoto ya upelekaji wa dawa za kutibu maji katika mtambo wa Ruvu Chini, ambapo kipindi cha mvua magari yanashindwa kufika.

Akijibu hilo, Mhandisi Mwakyusa alisema kuna mkandarasi ambaye ameifanyia marekebisho barabara, lakini mvua zinazoendelea zimesababisha barabara hiyo kuharibika mapema.

Marijani Gama alihoji kusuasua kwa barabara hiyo, huku akizigusia za Kibaha hadi njiapanda ya Baobab na ile ya Tanga Makurunge ambazo zimejengwa kwa awamu kwa kiwango cha lami, huku akihoji kutotekelezeka kwa barabara hiyo.

Awali, Mhandisi Mwakyusa aliwaambia wana CCM hao kwamba,  barabara hiyo kwa sasa ipo katika mpango na kwamba, wananchi 
wataopisha mradi huo watafanyiwa malipo, kauli iliyomuibua Usinga aliyehoji mpango huo.

"Mwenyekiti hii barabara kwa sasa bora kupanda pikipiki kuliko gari, adha yake ni kubwa kupita maelezo, mimi ni Diwani wa Yombo, wananchi wamefanyiwa tathmini mara kadhaa, lakini malipo bado kitendawili," alisema Usinga.

Aliongeza kwamba, "Tunaishauri Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), ingeijenga kwa lami kwa awamu, kuliko wanavyotumia pesa nyingi kila mwaka kuifanyia matengenezo yanayodumu kwa muda mfupi," alisema Usinga.

Akihitimisha mazungumzo hayo, Sharifu aliutaka uongozi wa RANROADS mkoani Pwani, Mhandisi Baraka Mwambage kuangalia umuhimu wa barabara hiyo inayounganisha wilaya na majimbo manne ambayo ni Bagamoyo, Kibaha Mji, Kibaha Vijijini na Kisarawe.

Mhandisi Mwakyusa aliwaambia wana CCM kwamba, amepokea ushauri huo na kwamba ata
uwasilisha kwa uongozi wa mkoa, ili kuona ni namna gani wanavyoweza kuufanyia kazi.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Halima Okash na viongozi wengine wakifuatilia maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Abdul Sharifu
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Bagamoyo, Aboubakary Mlawa na mmoja wa wana Sekretariet wakifuatilia kwa makini taarifa.
Abdul Sharifu akisisitiza jambo
Katibu Mwenezi Ramadhani Lukanga na Ibrahimu Gama wakiteta jambo

No comments