Header Ads

ad

Breaking News

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA ATUA NCHINI KWA ZIARA YA KITAIFA YA SIKU TATU

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (kushoto), akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali baada ya kuwasilini nchini kwa ziara ya siku tatu.

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali amewasili nchini leo Februari 29, 2024 kuanza ziara yake ya kitaifa ya siku tatu.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Waziri Mkuu Abiy amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba.

Mhe. Dkt. Abiy atapokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam Machi 1,2024.

Pamoja na mambo mengine, ziara ya Waziri Mkuu Abiy inalenga kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ethiopia katika maeneo ya kimkakati ikiwemo usafirishaji kwa njia ya anga, nishati, kilimo na mifugo, biashara na uwekezaji na ushirikiano katika sekta za elimu, uhamiaji, na ulinzi na usalama. Ziara hiyo ambayo itakamilika Machi 2, 2024 inafanyika kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan.   

No comments