Header Ads

ad

Breaking News

WATUMISHI OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZA WAPIGWA MSASA

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uwekezaji wa Umma, Fadhili Chilumba


MKURUGENZI Msaidizi Idara ya Uwekezaji wa Umma, Fadhili Chilumba kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji amefungua rasmi mafunzo ya Misingi ya Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma.

Akifungua mafunzo hayo, Chilumba amewataka watumishi kuzingatia mafunzo hayo ya maadili katika utumishi wa umma ili kutekeleza majukumu ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji katika kuleta matokeo chanya Kwa wananchi na wadau tunaowahudumia.

Mafunzo hayo ya awamu ya kwanza ya maadili katika utumishi wa umma yametolewa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Idara ya Usimamizi wa Maadili.

Mafunzo ya awamu ya pili kuhusu Kanuni za kudumu za utumishi wa umma yametolewa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala Sehemu ya Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Erasmo Mbilinyi.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala Sehemu ya Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Erasmo Mbilinyi

No comments