Header Ads

ad

Breaking News

WANAWAKE JKCI WAPONGEZWA KWA KULETA MAFANIKIO

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina akizungumza na wanawake wa Taasisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Machi 8.


Na Mwandishi Maalumu, Dar es Salaam

WANAWAKE wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wamepongezwa kwa kuwa sehemu kubwa ya kuleta mafanikio katika taasisi hiyo na kuifanya kujulikana kitaifa na kimataifa.

Pongezi hizo zimetolewa hivi karibuni na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo Asha Izina wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Asha alisema kutokana na huduma bora za matibabu ya moyo zinazotolewa na JKCI kumeifanya taasisi hiyo kujulikana duniani kote hivyo wanawake wa JKCI wawe mstari wa mbele kuhakikisha kuwa maendeleo hayo hayarudi nyuma.

Asha aliwataka wanawake wa Taasisi hiyo kuimarisha mshikamano eneo la kazi kwa kufuata miongozo ya utendaji kazi na kuleta ubora wa huduma kwa wagonjwa wanaowahudumia. 

“Sisi kama wanawake tuwe wakwanza kusimamia miongozo kuhakikisha kuwa mwanamke akipewa kazi ya kumhudumia mgonjwa aweze kumhudumia kwa kiwango cha juu na kuleta motisha kwa wengine kuiga mfano kwetu”, alisema Asha

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema maendeleo mengi yanayopatikana katika familia wanawake wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo hayo.

“Maendeleo makubwa ya Taasisi yetu yamefanywa na wanawake, kwani tangu taasisi hii ilivyoanzishwa idadi ya wanawake ni kubwa kuliko wanaume hivyo tunaamini mchango mkubwa hadi taasisi yetu kifikia hapa umefanywa na wanawake.

Aidha Dkt. Kisenge aliwashukuru wanawake wote wa JKCI kwa kuendelea kuleta upendo baina yao na kwa wagonjwa wanaowahudumia kwani wagonjwa wamekuwa wakifarijika kuona wanahudumiwa kwa upendo.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha wanawake JKCI Dkt. Angela Muhozya amewapongeza wanawake wa JKCI kwa kuwa chachu ya maendeleo katika jamii kwa kujitoa kila wanapohitajika kwaajili ya kuisaidia jamii.

“Wanawake wa JKCI wamekuwa mstari wa mbele kuisaidia jamii yetu kila tunapowahitaji kutoa huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo meeneo mbalimbali ya Dar es Salaam wakati wa kuadhimisha siku ya wanawake duniani”, alisema Dkt. Angela

Dkt. Angela alisema kuwa wanawake wa JKCI wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo misiba, shughuli za furaha na kuwezeshana kiuchumi kupitia mfuko wao waliouanzisha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwapongeza wanawake wa Taasisi hiyo kwa kazi nzuri wanayofanya wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa JKCI iliyopo jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina akimpatia Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge zawadi iliyotolewa na wanawake wa taasisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika taasisi hiyo hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpatia zawadi Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya JKCI, Asha Izina iliyotolewa na wanawake wa taasisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika taasisi hiyo hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya JKCI, Asha Izina pamoja na wawakilishi wa wanawake wa JKCI wakikata keki wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika taasisi hiyo hivi karibuni
jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
wakisikiliza wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika taasisi hiyo hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
wakisikiliza wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika taasisi hiyo hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika hivi karibuni katika taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Khamis Mussa

No comments