Header Ads

ad

Breaking News

WAKAMATWA WAKITOROSHA MADINI KILOGRAMU 9.8

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde (kulia), akiwa na kamanda wa polisi

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wafanyabiashara kumi wa madini kwa tuhuma za utoroshaji wa madini Kilogramu 9.8 yenye thamani ya shilingi 1,555,476,586

Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema wafanyabiashara hao walikamatwa Machi, 16, 2024, Jumamosi majira ya saa 10:27 alfajiri katika Mtaa wa Ilomba jijini Mbeya kwenye nyumba waliyokuwa wamepanga wakiwa na vipande 344 ya dhahabu iliyochomwa yenye uzito wa kilogramu 9.8 na vifaa mbalimbali kama vile Precious Metal analayzer (XRF) aina ya Niton DXL thermoscientific, mitungi ya gesi, jiko na vyungu kwa ajili ya kuchomea dhahabu, Kipimo cha maji cha kupimia dhahabu, mizani kadhaa pamoja na kemikali aina ya borax.

Mavunde ametoa rai kwa wafanyabiashara wote wa madini kuhakikisha wanazingatia sheria na kanuni za kufanya biashara ya madini nchini na kusisitiza kuwa wote watakaobainika kutorosha madini watachukuliwa hatua za kisheria pamoja na kufutiwa Leseni zao.

Aidha, Mavunde ameagiza kusimamishwa kwa leseni za biashara ya madini za watuhumiwa nchi nzima wakati taratibu za upepelezi zikiendelea kabla ya kufikishwa Mahakamani.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya wa Chunya, Mbaraka Batenga amewataka viongozi wote wa mitaa na vijiji kuwatambua watu katika maeneo yao kwa kuwasajili katika daftari la wakazi na kuwataka wamiliki wa nyumba za kupanga kuhakikisha wanawafahamu vyema wapangishaji wao na shughuli zao.

No comments