Header Ads

ad

Breaking News

TPHPA YAPATA MAFANIKIO, YAJIPANGA KUVUKA MALENGO

Profesa Joseph Ndunguru, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), akizungumza leo Machi 13, 2024.


Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Katika mwaka wa fedha 2023/2024 ilikasimia kukusanya kiasi cha fedha cha shilingi 6,454,437,453, mapato ya ndani (Owns Source) na katika kipindi cha miezi mitatu ya Julai  2023 hadi Septemba 2023, imekusanya shilingi 6,143,965 337.61 sawa na asilimia 95.2 ya makadirio ya makusanyo ya mwaka mzima  kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato ya ndani. 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Profesa Joseph Ndunguru, ameyasema hayo wakati wa kikao kazi kati ya mamlaka hiyo, wahariri na waandishi wa habari kilichofanyika leo Machi 13,2024 jijini Dar es Salaam.

Profesa Nduguru amesema kuwa, ni dhahiri kwamba hadi kufikia mwisho wa mwaka wa fedha, Mamlaka itaweza kukusanya zaidi ya asimilia 100 ya makadirio hayo na hivyo, kuweza kuongeza kiasi cha gawio lake kwa serikali kuu kwa asilimia 15 (Government Remitance) kutoka shilingi 968,165,000.62 walizotarajia hadi kufikia shilingi 3,686,379,202.56 kwa mwaka. 

"Hatua hiyo kwetu ni mafanikio makubwa, tutaendelea kufanya kazi kwa bidii ili tuweze kufikisha asilimia 100 ya makadirio au kuvuka lengo hilo, kwa pamoja tunaamini tutafikia na kuvuka lengo hilo," amesema Profesa Ndunguru.

Profesa Ndunguru amesema kwa upende wa ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali, katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2023, Mamlaka ilikusanya kiasi cha shilingi 5,352,196,967.04, wakati Januari hadi Machi 6,2024, Mamlaka imekusanya kiasi cha shilingi bilioni 3.7. 

Mkurugenzi mkuu huyo amesema kuwa, Mamlaka inatekeleza kwa vitendo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Msajili wa Hazina la kufanya mageuzi katika taasisi zake za Serikali ili kuleta tija kwenye taasisi zake.

Amesema sehemu yoyote yenye mafanikio, haikosi kuwa na changamoto, katika Mamlaka hayo ambazo ni pamoja na wafanyabiashara kutokuwa waaminifu na kushindwa kufuata sheria za mamlaka.

Changamoto nyingini ni kutokuwa na elimu ya kutosha kwa wadau wa viuatilifu na masuala ya afya ya mimea juu ya sheria, kanuni, miongozo na taratibu pamoja, uelewa mdogo wa jamii kuhusu majukumu ya Mamlaka mpya na mabadiliko ya tabianchi.

Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Profesa Joseph Ndunguru (kushoto) akizungumza na Mjumbe wa Kamati Uteendaji ya Jukwaa la Wahariri (TEF), Yasin Sadick.

Maofisa watendaji wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), wakiwa makini kuandika maswali kutoka kwa wahariri na waandishi wa habari.


Afisa Mwandamizi wa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri akieleza jambo wakati wa kikao kazi kati ya Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), na wahariri na waandishi wa habari kilichofanyika leo Jumatano Machi 13,2024, jijini Dar es Salaam.

Mhariri wa Tanzania Leo, Daniel Mbega, akiuliza swali

No comments