Header Ads

ad

Breaking News

TPHPA YAFANIKIWA KUDHIBITI NDEGE, WADUDU WAHARIBIFU WA MAZAO


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Viuatilifu Tanzania Tanzania (TPHPA), Profesa Joseph Ndunguru akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha na wahariri na waandishi wa habari leo Jumatano Machi 13,2024 jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), imefanikiwa kuwadhibiti ndege waharibufu wa mazao aina ya kweleakwelea wanaokadiriwa kufikia milioni 40 na na kufanikiwa kuokoa tani 5,675 mazao ya nafaka ya mpunga, mtama na alizeti. 

Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Profesa Ndunguru ameyasema hayo wakati wa kikao kazi kati ya Mamlaka hayo, wahariri na waandishi wa habari kilichofanyika leo Jumatano machi 13,2024, jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Ofisa ya Msajili wa Hazina.

Profesa Ndunguru amesema kuwa, kazi hiyo ya kuwadhibiti ndege hao waharibufu wa mazao imefanyika kwa kushirikiana na Shirika la Kudhibiti Nzige wa Jangwani (DLCO-EA), katika mikoa minne ya Morogoro, Tabora, Pwani na Manyara. 

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kuwa, ndege waharibifu hao walidhibitiwa katika maeneo yaliyotajwa kwa kunyunyizia kiuatilifu aina ya fenthion asilimia 60 ULV kwa kutumia ndege kwa njia ya anga na kwa kutumia vinyunyizi mbeleko vyenye injini kwa njia ya ardhini.

Kutokana na adha hiyo ya ndege waharibifu, Profesa Ndunguru amesema kuwa, TPHPA inaimarisha Kilimo Anga kwa kuongeza idadi ya ndege, ambapo mchakato wa ununuzi wa ndege mpya yenye thamani ya sh. bilioni 3, upo katika hatua ya mwisho. 

Amesema ndege hiyo italeta ufanisi katika udhibiti wa nzige na ndege jamii ya kwelea kwelea wanaoharibu mazao katika mikoa mbalimbali nchini.

Mkurugenzi mkuu huyo ameongeza kuwa, mamlaka imefanikiwa kudhibiti nzige wa kwenye miti Tree Locust waliokuwa wamevamia eneo lenye ukubwa wa hekta 1,248 katika kata ya Mtera na Chipogoro zilizopo Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma.

"Mamlaka tumefanikiwa kudhibiti wadudu wengine waharibu aina ya nzige kwenye miti, walivamia eneo kubwa katika kata za Mtera na Chipogoro wilayani Mpwapwani mkoani Dodoma," amesema Mkurugenzi mkuu huyo.

"Mamlaka ilipokea ndege nyuki moja aina ya  DJI Agras T40 kutoka Shirika la Kimataifa la Chakula (WFP) ambayo ina uwezo wa kubeba lita 40 za kiuatilifu na kunyunyizia hekari 52 kwa saa.

Ameongeza kuwa, Mamlaka imepokea ndege nyuki nyingine 20 kwa ajili ya kufanyia savei ya magonjwa na wadudu waharibifu wa mazao ili kuwadhibiti kabla ya kuleta madhara kwa kulima ili kuleta tija.

"Februari na Machi 2024, Mamlaka imefanikiwa kudhibiti visumbufu vya zao la alizeti aina ya Aphids, Viwavi na panzi katika ekari 495 za shamba la Building a Better Tomorrow (BBT ya Chinangali, Dodoma."

Profesa Ndunguru amesema kuwa, udhibiti huo umefanywa na Mamlaka Kwa kutumia drone ambayo ilinyunyuzia kiuatilifu aina ya Bamidacy Plus 344SE kwa ufanisi mkubwa na hivyo, kuchangia kuokoa upotevu wa zao hilo na hivyo kuchangia katika kuongeza tija.

Amesema ndege nyuki hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za uzalishaji ambazo zingetumika kuwalipa vibarua na kuokoa muda ambao ungetumika kufanya kazi hiyo kama ingafanywa na vibarua.

Ili kudhibiti mlipuko wa viwavi jeshi vamizi, lita 81,563 za Profenofos zimesambazwa katika  halmashauri 57 za mikoa ya Lindi, Pwani, Morogoro, Tanga, Geita, Manyara, Kilimanjaro, Dodoma, Singida, Dar es Salaam, Katavi na Arusha kwa ajili ya kudhibiti uharibifu unaotokana na viwavijeshi katika mazao ya nafaka. 

Mkurugenzi huyo amesema kuwa, lita 561 za Chlorpyrifos na Cypermethrin zimesambazwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, wakati jumla ya wakulima 2,987 na ugani 16 katika Kata 16 za Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.

"Mamlaka imefanikiwa kusajili jumla ya wadudu rafiki aina 11, kwani matumizi ya wadudu rafiki husaidia kupunguza matumizi ya viuatilifu vya viwandani."

Profesa Ndunguru amesema kwa upande wa udhibiti wa nzi wa matunda, jumla ya lita 585 za kiuatilifu aina ya Methyl Eugenol zimesambazwa katika wilaya mbalimbali nchini, ikiwemo Muheza (130) Handeni (60), Morogoro Mjini (45), Morogoro Vijijini (10), Bagamoyo (5), Pangani (25), Ubungo (30) na Shinyanga (5) kwa ajili ya kudhibiti nzi wa matunda ili kuongeza tija na ubora wa matunda.

Mafunzo ya mbinu za kudhibiti nzi wa matunda yalitolewa kwa wakulima 849 na maafisa ugani saba katika Wilaya ya Handeni katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 hadi Machi 2023.

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imeundwa kwa sheria ya Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Namba 4 ya 2020 (Plant Health Act. No. 4) kwa kuunganisha iliyokuwa Taasisi ya Utafiti wa viuatilifu ya Ukanda wa Kitropiki (TPRI) (Sheria Na. 18 ya 1979) na Kitengo Cha Afya ya Mimea kilichokuwa chini ya Wizara ya Kilimo (PHS) (Sheria Na.13 ya 1997).

Lengo la kuundwa kwake ni kuweka mfumo wa pamoja wa kisheria wa usimamizi na udhibiti wa afya ya mimea, mazao ya mimea na viuatilifu, ili kukidhi matakwa ya masoko na mikataba ya kimataifa (International Plant Protection Convention - IPPC) na kuweka Mazingira salama kwa Afya ya binadamu, Wanyama na Mimea kwa kuwa na matumizi sahihi na salama ya viuatilifu nchini.

Mkurugenzi mkuu huyo amesema TPHPA imeanza rasmi Julai 2022 ikitekeleza kwa vitendo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 

Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia Msajili wa Hazina la kufanya mageuzi katika Taasisi zake za Serikali (Reform, Rebuild, Resilience and Reconciliation (4Rs) ili kuleta tija kwenye taasisi zake.

Wahariri wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Viuatilifu Tanzania Tanzania (TPHPA), Profesa Joseph Ndunguru leo Jumatano Machi 13,2024 jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi wa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri akieleza jambo wakati wa kikao kazi.
Wahariri na waandishi wa habari wakifuatilia maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Viuatilifu Tanzania Tanzania (TPHPA), Profesa Joseph Ndunguru (hayupo pichani), leo Jumatano Machi 13,2024 jijini Dar es Salaam.

Maafisa wa Mamlaka ya Afya ya Viuatilifu Tanzania  (TPHPA)

No comments