Header Ads

ad

Breaking News

TAWA YAPATA MAFANIKIO, YATEKELEZA MPANGO MKAKATI

 

Kamishna wa Uhifadhi TAWA, Mabula Misungwi Nyanda akizungumza katika kikao kazi kilichiofanyika leo Jumatatu Machi 18,2024 jijini Dar es Salaam

Na Frank Balile

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA),  limefanikiwa kutekeleza mpango mkakati wa mamlaka wa mwaka 2021/22-2025/26 ambao ni kuimarisha ulinzi wa rasimali za wanyapori na malikale.

Akizungumza katika kikao kazi kati ya mamlaka hiyo, wahariri na waandishi wa habari, Kamishna wa Uhifadhi TAWA, Mabula Misungwi Nyanda, amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Samia Suluhu Hassan, TAWA kuboreshaji wa huduma za utalii na utendaji kazi wenye ufanisi na tija.

Nyanda amesema kuwa, malengo hayo yalitekelezwa na mafanikio makubwa yaliyofikiwa ni pamoja na ujangili wa tembo kupungua kutoka mizoga ya tembo 6 mwaka 2021/22 hadi mizoga watatu, Februari 2024.

Amesema mafanikio haya yanatokana kuimarika kwa ulinzi kulikochangiwa na kuongezeka kwa vitendea kazi, morali ya watumishi, mtandao kwa kiitelijensia, doria za mwitikio wa haraka matumizi ya teknolojia na kufunga visikuma mawimbi ili kufuatilia mienendo ya wanyamapori katika kuhakikisha wanyama wanakuwa salama.

Ametaja mafanikio mengine ni pamoja na Kupungua kwa migogoro mipaka kati ya Hifadhi na wananchi, huku wakiongeza ushirikiano na wananchi katika kutatua migogoro kwenye maeneo ya hifadhi kwa kutekeleza maelekezo ya Serikali yaliyotolewa kupitia Kamati ya Mawaziri nane wa Wizara za Kisekta.  

Kamishna wa Uhifadhi huyo amesema kuwa, kwa kushirikiana na wananchi, migogoro ya mipaka katika mapori ya akiba saba ya Swagaswaga, Mkungunero, Wamimbiki, Igombe, Liparamba, Mpanga Kipengere na Selous, kati hayo yaliyotolewa maelekezo na Kamati ya Mawaziri nane wa kisekta imemalizika.

Amesema kuwa, jumla ya vigingi 1,681 vimesimikwa kuzunguka mipaka ya hifadhi, ambapo katika utatuzi wa migogoro hiyo eneo lenye ekari 103,544.48 limemegwa  kutoka kwenye hifadhi na kuwapatia wananchi kwa ajili ya shughuli za kiuchumi.  

Ameongeza kuwa, sambamba na hilo, Serikali kupitia TAWA inaendelea kukamilisha zoezi la kulipa fidia kaya 145 zilizo katika Pori la Akiba Mkungunero.

Mafanikio hayo yanatokana kuimarika kwa ulinzi kulikochangiwa na kuongezeka kwa vitendea kazi, morali ya watumishi, mtandao kwa kiitelijensia, doria za mwitikio wa haraka matumizi ya teknolojia na kufunga visikuma mawimbi ili kufuatilia mienendo ya wanyamapori katika kuhakikisha wanyama wanakuwa salama.

Kufuatia juhudi hizo, madhara hasi ikiwemo idadi ya vifo imepungua kutoka vifo 318 kati ya mwaka 2017-2020 hasi vifo 259  kati ya mwaka 2021-2024 licha ya kuongezeka kwa matukio.

Amesema kuwa, kuliongeza ushirikishwaji jamii katika shughuli za uhifadhi na kuwezesha miradi ya maendeleo kwa Jamii.

Kamishna wa Uhifadhi huyo amesema kuwa, TAWA imeendelea kushirikiana na jamii katika shughuli za uhifadhi kwa kuchangia miradi ya maendeleo inayoibuliwa na jamii kwenye maeneo  mbalimbali hususan yanayozunguka Mapori ya Akiba. 

Nyanda amesema kati ya mwaka 2021 na 2024, TAWA imechangia miradi ya jamii yenye thamani ya Shilingi milioni  193.3 ambayo ni ujenzi wa Soko la samaki katika mji mdogo wa Ifakara – Kilombero shilingi milioni 66.

Ametaja miradi mingine ni ujenzi wa darasa, ofisi ya walimu na ununuzi wa madawati katika Shule ya Msingi Usinge Kaliua mkoani Tabora (shilingi Milioni 50, pamoja na kuchangia madawati 100 katika Wilaya ya Bunda.

 Nyanda ameongeza kuwa, ununuzi wa mashine mbili za Kusaga katika Mkoa wa Mara, kuchangia shilingi milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati na darasa-Mwibara na kuchangia shilingi milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Bungo iliyopo wilayani Korogwe mkoani Tanga. 

Afisa Mwandamizi wa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri akieleza jambo wakati wa kikao kazi.
 Maofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), wakifuatilia wasilisho la Kamishna wa Uhifadhi TAWA, Mabula Misungwi Nyanda (hayupo pichani), kwa wahariri na waandishi wa habari katika kikao kazi kilichoratibiwa na Ofisa ya Msajili wa Hazina leo Jumatatu Machi 18,2024.
Baadhi ya wahariri wakifuatilia wasilisho
Baadhi ya wahariri

No comments