Header Ads

ad

Breaking News

TANZANIA YAUZA TANI 560,000 ZA ASALI, TAWA YAJIPAMBANUA

Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo, akielezea mipango yao kwa wahariri na waandishi wa habari wakati wa kikao kazi kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam leo Jumanne Machi 19,2024.


Na Mwandishi Wetu

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), umesema katika kipindi cha miaka mitatu iliyipita Tanzania imeuza jumla ya tani elfu 5.6 za asali nje ya nchi yenye thamani ya Marekani milioni 40.

Akizungumzia mafanikio ya TFS katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo, hayo ni mafanikio makubwa kwa Wakala wa Huduma za Misitu.

Akiwa kwenye kikao kazi kilichowakutanisha TFS, wahariri na waandishi wa habari, Profesa Silayo amesema asali ya Tanzania hupimwa katika maabara za kimataifa za ithibati kila mwaka na katika kipindi chote cha miaka mitatu tumepata alama za juu wastani asilimia 96/100.

"Asali yetu ni bora sana, kwanza hupimwa katika maabara za kimataifa za ithibati kila mwaka, katika kipindi chote hicho tumepata alama za juu za wastani wa asilimia 96/100, kwetu ni mafanikio makubwa sana," amesema Profesa Dos Santos Silayo.

Prosesa Silayo amesema kuwa, masoko makubwa ya bidhaa hiyo yanapatikana katika nchi za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, Uarabuni, Marekani na Afrika Mashariki (EAC) na nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Ameongeza kwamba, kupitia mashindano ya ubora wa asali zinazozalishwa barani Afrika, asali ya Tanzania iliyozalishwa mkoani Tabora ilishika nafasi ya pili kwa ubora.

"Asali iliyozalishwa mkoani Tabora, ilishika nafasi ya pili kwa ubora kwenye mashindano ya ubora wa asali inayozalishwa Afrika," amesema Profesa Silayo.

Profesa Silayo amesema uwezo wa kuzalisha (potential) ni 138,000t asali na nta 9,200t kwa mwaka, lakini hali ya sasa uzalishaji ni 30,000t za asali na tani 1,843 za nta kwa mwaka, zikizalishwa na wafugaji milioni 1.2, wakati makundi (colonies) milioni 10.

Amesema uzalishaji wa mazao ya nyuki nchini umeongezeka hadi kufikia wastani wa tani elfu 32,691 kutoka tani 31,179 sawa na ongezeko la asilimia 5.

Akizungumzia viwanda vya mazao ya nyuki, amesema watahakikisha wanatekeleza ujenzi wa kiwanda kipya cha kuchakata asali wilayani Nzega mkoani Tabora, kukarabati viwanda vingine viwili wilayani Manyoni mkoani Singida na kingine katika shamba la miti Saohill mkoani Iringa.

Kamishna wa Uhifadhi huyo ameweka wazi mauzo ya mazao ya misitu nje ya nchi, kuwa, yaliongezeka kwa asilimia 87 kutoka meta za ujazo 227,615 mwaka 2020/21 hadi meta za ujazo 426,805 kwa mwaka 2022/2023, wakati kwa upande wa mbao zolizohandisiwa, mauzo nje yaliongezeka kutoka meta za ujazo 15,876 hadi 47,491 ni sawa na asilimia 66.6.

"Viwanda vya kati hadi vikubwa viliongezeka kutoka 6,029 hadi 7,356 sawa na asilimia 18, vinajumuisha vidogo vya kutengeneza samani, uchakataji mbao, utengenezaji bidhaa zilizohandisiwa ikiwemo marine boards, veneer, viwanda vya nishati ya mkaa, viwanda vya nguzo na viwanda vikubwa vya kutegeneza karatasi," amesema Profesa Silayo.

Amesema kuwa, TFS kwa kushirikiana na Mfuko wa Misitu (TaFF), ulikamilisha ujenzi wa viwanda vipya vitano vilivyojengwa katika Wilaya za Mlele, Kibondo, Sikonge, Tabora na Bukombe, ikiwa ni ongezeko kutoka viwanda 38 hadi 97.

Profesa Silayo amesema kuwa, TFS ilishiriki vyema katika miradi mbalimbali ya kimakati ya taifa, ambayo ni miradi hiyo ni mkatati wa kuifanya Dodoma kuwa Kijani na kusafisha eneo la mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP).

Amesema katika kuunga mkono uamuzi wa Serikali wa kuhamia Dodoma, TFS kwa kushirikiana na Jiji la Dodoma, VPO na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi waliazimia kutekeleza kwa pamoja mpango wa kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.

"Lengo la mpango huo wa kuifanya Dodoma kuwa ya kijani ni kuzuia mmomonyoko wa udongo, uharibifu wa mazingira, kuongeza uoto na kupendezesha mandhari ya Jiji la Dodoma na vitongoji vyake.

Amesema kuwa, miche 2,792,200 ilikuzwa na kupandwa katika eneo sawa na hekta 6,175, nyasi za aina mbalimbali zilipandwa mahsusi katika jiji hilo kama vile Mji wa Serikali, wakati miche 2,792,200 ilikuzwa na kupandwa katika eneo sawa na hekta 6,175.

Profesa Silayo amesema nyasi za aina mbalimbali zilipandwa katika mahsusi katika jiji hilo kama vile Mji wa Serikali, huku akieleza mikakati yao ya baadaye ya kuongoa na kuzuia uharibifu wa misitu kwa kiasi cha hekta milioni 5.2 kufikia 2030.

"Tutaongeza upatikanaji wa malighafi ya viwanda vya misitu kwa kupanda miti na kuongeza mashamba ya miti na kuimarisha utalii ikologia na utalii wa nyuki, hii itachangia kuongezeka kwa mapato ya taasisi kwa kupanua wigo wa vyanzo vya mapato ikiwa ni pamoja na fursa za biashara ya kaboni," amesema.

Kamishna wa Uhifadhi huyo amesema mikakati yao mingine ni kuhakikisha wanatatua migogoro ya misitu na wadau wengine hasa vijiji pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa kushirikisha jamii.

Amesema watahakikisha wanaimarisha ubora na mnyororo wa thamani wa mazao ya nyuki, kutafuta masoko ya bidhaa za nyuki na kuboresha huduma za nyuki katika mifumo ikologia mfano kutumia kwenye uchavushaji wa mazao.

Profesa Silayo amesema sekta ya misitu na nyuki nchini ni muhimu kutokana na mchango wake mkubwa katika ukuaji wa sekta nyingine za uzalishaji kama utalii, maji, kilimo, mifugo na nishati na sekta ya viwanda.

Amesema kutokana na umuhimu huo, uhifadhi wa rasilimali za misitu ni jukumu la msingi na linapaswa kupata mchango kutoka kwa wadau wote, hivyo ameitaka jamii kuwa nao katika safari hii ya uhifadhi wa rasilimali za misitu kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vya baadaye, wajiepushe na kuchoma moto misitu na uvunaji haramu.

Wahariri akifuatilia taarifa ya TFS
Wahariri akifuatilia taarifa ya TFS


Afisa Mwandamizi wa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri akieleza umuhimu wa kikao kazi.

Wakisikiliza taarifa iliyokuwa ikitolewa na Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo
Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo (kulia), na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Salim Said Salim wakisikiliza maswali

No comments