Header Ads

ad

Breaking News

SIMBA SC YATINGA ROBO FAINALI KIBABE, YAIGAGADUA JWANENG GALAXY 6-0

 


Na Mwandishi Wetu
WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC, wametinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kibabe zaidi, baada ya kuwagagadua 
Jwaneng Galaxy ya Botswana mabao 6-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi B, uliopigwa leo Jumamosi Machi 2,2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yamefungwa na Saido Ntibazonkiza dakika ya saba, Pa Omar Jobe dakika ya 14, Kibu Denis Prosper dakika ya 22, Clatous Chama dakika ya 76, Ladack Chasambi dakika ya 86 na Fabrice Ngoma dakika ya 89.

Simba SC imemaliza ya pili kwenye Kundi B ikiwa na pointi tisa sawa na Wydad Casablanca, wote wakiwa nyuma ya ASEC Mimosas iliyojikusanyia alama 11.

Kwa matokeo hayo, Mnyama ametinga hatua ya robo fainali kwa faida ya mechi zao mbili, huku Simba ikiibuka na ushindi wa jumla dhidi ya Wydad baada ya kufungwa bao 1-0 ugenini nchini Morocco na kushinda mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Pamoja na faida hiyo, Simba wana wastani mkubwa zaidi wa mabao dhidi ya timu ya Casablanca.


No comments