Header Ads

ad

Breaking News

RC MWASSA AWASIHI WANANCHI KUTOCHAFUA ZIWA VICTORIA

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajat Fatma Mwassa akizungumza na wananchi na wadau wa usafirishaji wanaofanya shughuli ndani ya Ziwa Victoria

Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Mkoa wa Kagera, Hajat Fatma Mwassa amewataka wananchi na wadau wa usafirishaji wanaofanya shughuli ndani ya Ziwa Victoria, kutofanya yote yanayoweza Kuathiri au kusababisha uchafuzi wa Ziwa Victoria ili kuendana na mpango wa Taifa wa kupambana na vitendo hivyo, ikiwemo umwagikaji wa mafuta ziiwani na baharini.

RC Mwassa ameyasema hayo wakati wa warsha ya mafunzo ya siku tatu yaliyoandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Kagera Machi 20, 2024 yenye lengo la Kudhibiti Vitendo vya umwagikaji mafuta ndani ya Ziwa, akiwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo, Mkuu wa Mkoa huyo ameeleza kwamba, mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa eneo la Mkoa Kagera kwa kuwa Ziwa Victoria linagusa wilaya za Mkoa wa Kagera, hivyo utunzaji wa Ziwa unagusa sana jamii watu  wa Kagerakwakuwa maji haya hutumika kunywa, kula na shughuli nyingine za kibinadamu na kugusa hadi mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa.

RC Mwassa amesisitiza kuwa, shughuli nyingine za uvuvi zimekuwa zikifanyika ziwani humo, endapo vitendo vya umwagaji mafuta katika Ziwa havitachukuliwa hatua za kupambana navyo, itasababisha kukosekana kwa mazao ya samaki na samaki wenyewe kama kitoweo, hii itaathiri upatikanaji wa samaki bora ikiwa ni Pamoja na kupungua kwa pato la mtu mmoja mmoja (mvuvi) na pato la Taifa, huku akitolea mfano Wilaya ya Muleba ambayo kwa asilimia kubwa mapato ya halmashauri hiyo hutegemea Shughuli za uvuvi hasa dagaa.

Amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa, mabalozi wazuri wa mapambano hayo na kuwa yale watakayofundishwa na kujifunza yakawe chachu ya kuendelea kudhibiti na kukomesha Pamoja na kushughulikia matendo kama hayo ya uchafuzi na umwagaji mafuta ziwani pale yatakapojitokeza.

Mafunzo hayo muhimu kwa maslahi ya Taifa, ambayo ni mpango wa Kitaifa wa kudhibiti uchafuzi wa maziwa na bahari kwa umwagaji wa mafuta yamekuja wakati ambao nchi jirani za Uganda na Kenya, zipo katika mchakato wa hatua za uchimbaji wa mafuta ziwani, ambapo Shughuli ikikamilika ya uchimbaji, mafuta hayo yatasafirishwa.


No comments