Header Ads

ad

Breaking News

RAIS SAMIA ASHIRIKI MAZISHI YA RAIS MSTAAFU MZEE ALI HASSAN MWINYI, MANGAPWANI ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine mbalimbali wakiomba Dua ya pamoja kabla ya mazishi ya  Rais mstaafu wa awamu ya pili hayati mzee Ali Hassan Mwinyi yaliyofanyika kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja, Machi 2,2024.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Viongozi mbalimbali wakiswali  swala ya maiti mbele ya jeneza lenye mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili hayati mzee Ali Hassan Mwinyi kabla ya kuzikwa kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja, Machi 2,2024.

Bibi Siti Mwinyi Mjane wa Rais mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi na Familia yake wakiwa katika Simanzi na majonzi wakati Jeneza lenye mwili wa hayati mzee Mwinyi likitolewa mara baada ya kuswaliwa kuelekea kwenye makaburini kwa ajili ya mazishi yaliyofanyika kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja, Machi 2,2024.

Viongozi wastaafu mbalimbali wakiwa katika kisomo na dua kabla ya mazishi ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili hayati mzee Ali Hassan Mwinyi yaliyofanyika Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja, Machi 2,2024.

No comments