Header Ads

ad

Breaking News

RAIS DKT.SAMIA ATANGAZA SIKU 7 MAOMBOLEZO KIFO CHA RAIS MSTAAFU MWINYI

RAIS Samia Suluhu Hassan ametangaza siku saba za maombolezo kuanzia kesho kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia leo katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu ya saratani ya mapafu.

Akitangaza kutokea kwa kifo hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema, Rais Mstaafu Mwinyi amefariki saa 11:30 jioni wakati akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.

“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania natoa pole kwa familia, ndugu jamaa na marafiki na watanzania wote kutokana na msiba huu mkubwa, aidha natangaza siku saba (7) za maombolezo, ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia kesho Machi 1,2024,” ametangaza Dkt. Samia.

No comments