Header Ads

ad

Breaking News

MABORESHO NHIF YACHANGIA MAFANIKIO, WAJA NA MKAKATI MZURI

Mkurugenzi Mkuu  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF),  Bernard Konga, akielezea mafanikio ya mfuko huo katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita, wakati wa mkutano wa wahariri na waandishi wa habari uliofanyika leo Machi 7,2024 jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mkuu wa  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga, amesema mfuko huo umepata mafanikio makubwa baada ya kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa kuzingatia mahitaji halisi ya tiba kwa sasa. 

Konga amesema kuwa, maboresho yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan yamechangia sana mafanikio ya NHIF, huku wakiendelea kuboresha kitita chake na kutoa kitita cha mafao chenye wigo mpana ukilinganisha na skimu nyingine za bima ya afya.

Mkurugenzi huyo ametoa kauli hiyo alipokutana na wahariri na waandishi wa habari leo Machi 7,2024 jijini Dar es Salaam, ambapo aliwaeleza mafanikio ya mfuko huo katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Dkt.Samia,kumekuwa na mabadiliko kwenye ugharamiaji wa huduma za kibingwa na bobezi, akitolea mfano 

gharama za wagonjwa wa saratani kwa mwaka 2023/2023 ilikuwa shilingi bilioni 32.46, ukilinganisha na shilingi bilioni 12.25 kwa mwaka 2021/2022, huku maradhi ya figo gharama zikiwa shilingi bilioni 35.40 na shilingi bilioni 11.45 mtawalia,” amesema Konga.

Konga amesema serikali inatimiza wajibu wake Kikatiba kuhakikisha wananchi wanakuwa na uhakika wa kupata huduma bora za afya, na kwamba sheria zilizopo zikiweka uhiari wa wananchi katika sekta isiyo rasmi na sekta rasmi ya binafsi kujiunga na bima ya afya, hatua ambayo husababisha wengi kujiunga wakiwa tayari na matatizo ya kiafya.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kuwa, uhalisia unaonesha asilimia 85 ya wananchi hawana Bima ya Afya, hivyo hukosa uhakika wa huduma bora za afya wakati wanapohitaji hufduma hiyo.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati ya utendaji kutoka jukwaa la wahariri Tanzania (TEF),  Said Salim Said aliwapongeza NHIF kwa kutekeleza wajibu wao kwa kuendelea kuelimisha umma namna ambavyo wanafanya kazi zao kwa ufanisi.

Kuhusu Bima kwa Wote, Konga amesema sheria inataka kila mkazi na raia kuwa na bima ya afya, wakati wananchi wasio na uwezo watagharamiwa bima ya afya na Serikali kupitia vyanzo muhsusi vya mapato yatakayowekwa katika akaunti maalum.

Amesema wataendelea kutoa elimu kwam umma kuhusu dhana na umuhimu wa kuwa na bima ya afya, huku wakiimarisha matumizi ya TEHAMA katika utambuzi, usajili wa wanachama, ukusanyaji wa michango, uwasilishaji, uchakataji na ulipaji wa madai (Artificial Intelligence).

Mkurugenzi huyo amesema kuwa, wanaendelea na mipango yao ya kuimarisha upatikanaji wa huduma bora kwa wanachama kwa kuendelea kutoa mikopo ya vifaa tiba, ukarabati/ujenzi  na dawa, kuboresha muundo wa shirika ili kukidhi mahitaji ya utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.

Amesema kuwa, wataongeza wigo wa mtandao wa vituo vya kutolea huduma za afya, pamoja na kushirikisha wadau mbalimbali kwa lengo la kuimairisha uhusiano mwema na wadau wote na Kuendelea kuimarisha uhai na uendelevu wa Mfuko.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Thobias Makoba, akizungumza alipokuwa akitoa neno la utangulizi mapema kabla ya Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga kutoa wasilisho lake katika mkutano huo.
Wahariri wakisiliza wasilisho 
Wahariri na waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Anitha Mendoza (kuli), pamoja na wahariri na waandishi wa habari wakisiliza taarifa ya NHIF.
Wahariri na waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini

Mkurugenzi Mtendaji wa Fullshangwe Blog, John Bukuku akiuliza swali katika mkutano NHIF na wahariri.
 Afisa Mwandamizi wa Uhusiano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri, akifafanua jambo
Wakifuatilia wasilisho
Mjumbe wa Kamati Tendaji TEF, Salim Said Salim akizungumza alipokuwa akitoa neno la shukrani mapema kabla ya kuhitimishwa kwa mkutano huo.(PICHA ZOTE NA HUGHES DUGILO)

No comments