Header Ads

ad

Breaking News

DKT.SAMIA AMEMALIZA KAZI - MBUNGE MGALU

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu


Na Omary Mngindo, Bagamoyo

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu, amesema hoja zinazoibuliwa na viongozi wa Chamacha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika maandamano yao, tayari Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amezifanyia kazi.

Mgalu alitoa kauli hiyo kwenye Jukwaa la Maridhiano Tanzania (JMAT), lililohudhiliwa na viongozi wa dini mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa kamati hiyo Taifa Dkt.Alhad Musa Salum, lililofanyika Bagamoyo mkoani Pwani.

Alisema kuwa, pamoja na lengo zuri la viongozi hao la kutaka kuihimiza Serikali katika masuala mbalimbali, lakini Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya Rais msikivu Dkt.Samia mambo mengi yanayodaiwa na wanasiasa hao, yamefanyiwa kazi na mengine yanaendelea kutekelezwa.

"Niwaombe viongozi wa CHADEMA wasitishe maandamano kwani wanayoyalalamikia tayari Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameyafanyia kazi, mengine anaendelea nayo ikiwemo ya mabadiliko ya katiba na tume huru ya uchaguzi," alisema Mgalu.

Aliongeza kwamba, "Maandamano ni haki ya kikatiba, vyama vimeomba na kukubaliwa, lakini hoja wanazoziibua tayari zimepatiwa majibu, huku nyingine zikiendelea kushughulikiwa," alisema mbunge huyo.

Akizungumzia Katiba mpya, Mgalu alisema kwamba, Rais alitangulia kuitolea taarifa Januari 3, 2023, kupitia mkutano uliohusisha viongozi wa vyama vya siasa, alitangaza wazi kuwa serikali ipo tayari kuanza mchakato wa Katiba mpya," alisema Mgalu.

"Mchakato wa Katiba kuna kikosi kazi kinachoendelea na taratibu zake, sanjali na maridhiano yatayokuwa na makubaliano kwenye kikosi hicho kitachokuwa na mchakato wa uundaji wa Sheria tatu ikiwemo mchakato wa tume huru ya uchaguzi," alisema.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ngazi ya Taifa Dkt.Alhad Musa Salum alizungumzia majukumu ya viongozi wa dini, akiwakumbusha watanzania kuhakikisha chaguzi zinazokuja zinafanyika kwa amani na usalama.

Naye, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Abdul Sharifu aliwataka viongozi wa dini kutumia nyumba za ibada kuhimiza amani, upendo na mshikamano maana Tanzania ni ya wa Tanzania.

No comments