Header Ads

ad

Breaking News

DKT.NCHIMBI AWASILI ZANZIBAR KUSHIRIKI MAZISHI YA MZEE MWINYI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi (kushoto), akisalimiana na Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Dkt.Abubakar Zubeir Bin Ally, walipokutana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume. 

Dkt.Nchimbi amewasili Zanzibar leo Jumamosi, Machi 2, 2024, akitokea nchini India, ambapo amelazimika kukatisha ziara yake ya kikazi ili kushiriki msiba wa Mwenyekiti wa CCM mstaafu na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi.




 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiongoza wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Awamu ya Pili, Hayati Alhaj Ali Hassan, Jumamosi, Machi 2, 2024, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akimpa pole Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi (Mb), ambaye ni mmoja wa watoto wa hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi, baada ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa hayati Mwinyi, Machi 2, 2024, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akimpa pole Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Hussen Ali Mwinyi (kulia), ambaye pia ni mmoja wa watoto wa Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi, baada ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili Hayati Mwinyi, Machi 2, 2024, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akimpatia pole mmoja wa Wajane wa Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Bi. Siti Mwinyi (aliyekaa), baada ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Hayati Mwinyi, shughuli iliyofanyika Jumamosi, Machi 2, 2024, kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi akiweka mchanga kwenye kaburi, wakati wa mazishi ya aliyekuwa  Mwenyekiti wa CCM na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  wa Awamu ya Pili, hayati Ali Hassan Mwinyi, aliyezikwa leo Jumamosi Machi 2,2024 Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.



No comments