Header Ads

ad

Breaking News

DAR YAONGOZA KUWA NA KASINO NYINGI, YASAJILI KAMPUNI 91

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), James Mbalwe akielezea mambo mbalimbali ya bodi hiyo.


Na Mwandishi Wetu

BODI ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, imesema kuwa, Dar es Salaam inaongoza kwa kuwa na kasino nyingi kuliko mikoa mingine hapa nchini.

Akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha maofisa wa Bodi hiyo, waandishi na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo Machi 6,2024, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, James Mbalwe amesema Dar es Salaam zipo kasino nane, wakati Arusha na Mwanza kila mkoa zina kasino moja.

"Dar es Salaam inaongoza kwa kuwa na kasino nane, wakati Mwanza na Arusha kila mkoa una casino moja, sawa na asilimia 90 ya kasino zipo Dar es Salaam," amesema Mbalwe.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa, kuna aina mbalimbali ya michezo ya kubahatisha ambayo ni michezo ya kibiashara kama kasino inayochezwa kwenye majumba maalum na mtandaoni, slot inayochezwa zaidi kwenye maduka maalum na baa, ubashiri wa matokeo ya michezo mtandaoni na madukani na bahati nasibu ya jumbe fupi za simu (sms lotteries).

Nyingine ni maduka ya mashine Arobaini, Bahati Nasibu ya Taifa, michezo isiyo ya Kibiashara, Promotional Lotteries na Public Lotteries ambayo hufanyika kwa vipindi vifupi vifupi kwa malengo maalum.

Amesema hadi kufikia Juni 2023, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), imesajili jumla ya kampuni 91 zinazoendesha biashara aina mbalimbali ya michezo ya kubahatisha nchini.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kuwa, kampuni moja inaweza kuendesha zaidi ya aina moja ya michezo ya kubahatisha, kwani leseni zote ni za muda wa mwaka mmoja isipokuwa  ile ya kuendesha BNT ambayo ni ya miaka minane na leseni uhuishwa baada ya muda wake kumalizika.

Mbaga amesema kuwa, watoto wenye umri chini ya miaka 18 hawarusiwi kushiriki michezo ya kubahatisha, mwendeshaji sharti awe na leseni hai iliyotolewa na GBT, michezo hairuhusiwi kuendeshwa katika maeneo yaliyo Karibu na nyumba za ibada, shule, usalama, yasiyofikika kirahisi na maeneo ya kuendeshea biashara ya michezo ya kubahatisha sharti yawe yamesajiliwa.

Amesema kuwa, mchango wa sekta katika mapato ya serikali kodi imeongezeka kutoka shilingi bilioni 33.6 mwaka 2016/17 hadi kufikia shilingi bilioni 170.4 kwa mwaka 2022/23, ambapo ni sawa na ongezeko la wastani wa asilini 407.1 kwa mwaka katika kipindi hicho.

"Sekta ya michezo ya kubahatisha Tanzania tumefanikiwa kuzalisha ajira zilizo rasmi na zisizo rasmi zaidi ya 25,000. Hivyo sekta hii imefanikiwa kutoa mchango mkubwa katika uzalishaji wa ajira nchini," amesema Mkurugenzi mkuu huyo.

Ameongeza kuwa, mapato ya Serikali yatokanayo na Kodi ya biashara ya michezo ya kubahatisha yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka.

Mkurugenzi mkuu ameyataja mafanikio waliyopata ni pamoja na kuchangia Mfuko Mkuu wa Hazina, kupata hati safi ya ukaguzi tangu kuanzishwa kwake, Tanzania kuwa mfano kwa baadhi ya nchi za Afrika, hususan ukanda wa mashariki, kati na kusini isipokuwa Afrika Kusini na kuwa mwalimu kwa baadhi ya nchi zikiwemo Kenya, Uganda, Zimbabwe, Malawi na Ethiopia.

Kwa upande wa michezo, Mkurugenzi Mkuu wa GBT, amesema kuwa, sekta hiyo inachangia maendeleo ya michezo nchini ambapo asilimi 5 ya kodi yote inayokusanywa kutoka katika Michezo ya Kubashiri Matokeo (Sports Betting), hupelekwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa ajili ya kusaidia kukuza michezo nchini.

Sabato Kusori kutoka ofisi ya Msajili wa Hazina akifafanua jambo kwa wahariri na waandishi wa habari wakati wa kikao kazi cha Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), kililichoandaliwa na ofisi ya Msajili wa Hazina leo Machi 6,2024 jijini  Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Daniel ole Sumayan, akijibu maswali yaliyoulizwa na wahariri katika kikao kazi kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina leo Machi 6,2024.
Wahariri wakisikiliza kwa makini


No comments