Header Ads

ad

Breaking News

CCM Bagamoyo kuanza kumnadi Some

Na Omary Mngindo, Bagamoyo

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani kikishirikiana na viongozi mbalimbali wakiwemo wa chama hicho ngazi ya wilaya kinataraji kuanza kampeni ya kumnadi Mrisho Some katika uchaguzi mdogo wa udiwani.

Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni ni wa kujaza nafasi iliyowazi, ambapo kwa mkoa huo kuna nafasi tatu kwenye majimbo ya Kibiti, Bagamoyo na Kibaha Mji.

Akizungumza ofisini kwake, Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Abdul Sharifu alisema uzinduzi wa kampeni hiyo utafanyika Machi 15,2024 kwenye Kijiji cha Fukayosi.

"Niwaombe wana Fukayosi kujitokeza kwa wingi katika mikutano yetu ya kampeni, siku ya kupiga kura mjitokeze kwa wingi kumchagua Mrisho Some ili awe diwani wetu wa Kata ya Fukayosi," alisema Sharifu.

Kwa upande wake Some, aliwashukuru viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya wilaya mpaka mkoa kwa kuona anafaa katika kinyang'anyiro hicho cha uchaguzi mdogo wa kata hiyo.

"Kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya njema anayoendelea kunijaalia, pia nawashukuru viongozi wangu wote wa chama changu kuanzia ngazi ya wilaya na mkoa kwa kulikubali jina langu," alisema Some.

Uchaguzi mdogo katika kata hizo tatu zilizopo majimbo ya Kibiti, Kibaha Mji na Bagamoyo ni wa kujaza nafasi za madiwani waliotangulia mbele za haki, ambapo Fukayosi aliyekuwa diwani wao Ally Ally alifariki miezi michache iliyopita.


No comments